Akizungumza katika Mkutano huo,Mkuu wa Wilaya alisisitaza mambo yafuatayo:
Mauaji ya akina Mama Undomo
Alisema kuwa suala hili halivumiliki na kwamba hatua za kisheria zitazidi kuchukuliwa kwa wale wanaokiuka sheria.
Suala la migogoro ya ardhi:
Alisema kuwa hategemei kuona migogoro mipya ikiibuka.kamati maalum ishaundwa kwaajili ya kushughulikia migogoro ya ardhi.Nataka kuona migogoro ya kihistoria tu na si mipya,alisema Mkuu wa Wilaya.
Maji:
Alifafanua kwamba sasahivi kuna tatizo la maji Katika Halmashauri ya mji Nzega kutokana na Bwawa la Uchama linalotegemewa kwa kiasi kikubwa na wakazi wa Nzega kukauka.Aidha alisisitiza kuwa mradi wa Maji wa Ziwa Victoria umeshaanza kwani mkandarasi tayari yuko site.
Elimu:
Kwa matokeo ya Mwaka jana kwa shule za Msingi Halmashauri ya Mji Nzega ilishika nafasi ya pili kimkoa kwa asilimia 72.Hivyo jitihaza ziongezwe ili matokeo yajayo tuwe wa kwanza,alisema Mkuu wa Wilaya.Aidha alieleza kuwa Halmashauri ya Mji Nzega itakuwa na shule ya kidato cha tano na sita katika shule ya Sekondari Bulunde na kwamba Wanafunzi wameshaanza kuripoti.Tunaendelea pia na Ujenzi wa shule kubwa ya bweni ya Wasichana inayojengwa katika Kata ya Mwanzoli.Tunaamini baada ya mda mfupi shule hii itakuwa imekamilika.Alisema Mkuu wa Wilaya .
Afya:
Sekta ya Afya imezidi kuimarika na kwamba tatizo la dawa litaisha kwani Serikali itakuwa na zabuni ambaye ikitokea MDS wakachelewesha basi mzabuni ataleta dawa.Alisisitiza pia kuwa hospitali zote za Wilaya ziwe na duka la Dawa.
Mkuu wa Wilaya pia alizungumzia mambo mengine ikiwemo,upandaji wa miti,barabara nk.
NZEGA TOWN COUNCIL (HALMASHAURI YA MJI NZEGA)
Sanduku la Barua: S.L.P 256 NZEGA-TABORA
Simu ya Mezani: +255677003373
Simu ya Mkononi: +255677003373
Barua Pepe: td@nzegatc.go.tz
Haki miliki zote zimehifadhiwa na nzegatc 2017