BI.LEAH KATAMBA AHIMIZA MASOMO YA SAYANSI KWA VITENDO
Afisa Elimu Sekondari Mji wa Nzega Bi.Leah Katamba amewahimiza walimu kujikita hasa kwenye matumizi ya vitendo katika kufundisha masomo ya sayansi
akiwa katika Mashindano ya club za sayansi yaliyo fanyika kwenye ukumbi wa Shule ya Sekondari Bugwagoso yaliyo shilikisha shule zote za sekondari.Bi Leah amesema naona jitihada kubwa munazo zifanya kwenye mashule ambapo hapa naona watoto wameonyesha uwezo wao wakubuni mambo mbali mbali ya kisayansi hivyo nendeni mkaendelee kujikita katika masomo ya sayansi kwa vitendo.
Idara ya Elimu sekondari Mji wa Nzega wamekuwa na taratibu ya kuendesha mashindano ya masomo ya sayansi ili kuwafanya wanafunzi waendelee kulipenda somo la sayansi
NZEGA TOWN COUNCIL (HALMASHAURI YA MJI NZEGA)
Sanduku la Barua: S.L.P 256 NZEGA-TABORA
Simu ya Mezani: +255677003373
Simu ya Mkononi: +255677003373
Barua Pepe: td@nzegatc.go.tz
Haki miliki zote zimehifadhiwa na nzegatc 2017