Chimbuko/asili
Utangulizi
Halmashauri ya mji wa Nzega ni Sehemu ya Wilaya ya Nzega Mkoa wa Tabora na ilianzishwa mwaka 2014.Halmashauri ya Mji wa Nzega ni mojawapo ya Halmashauri 8 za Mkoa wa Tabora, ambazo ni Halmashauri ya Wilaya ya Nzega, Manispaa ya Tabora, Urambo, Kaliua, Sikonge, Uyui, na Igunga.
Wakazi wa Halmashauri ya Mji wa Nzega ni mchanganyiko wa makabila mbalimbali ambayo ni wasukuma, wanyamwezi, waha na wanyiramba. Kabila ambalo ni wenyeji wa Halmashauri hii ni Wasukuma. Nzega ilipanda kufikia hadhi ya kuwa mamlaka ya Mji mdogo mwaka. Kasi ya kupanuka kwa Mji wa Nzega iliongezeka kidogo kidogo na ilipofika tarehe 12/9/2014 ikapanda hadhi na kuwa Halmashauri ya Mji. Kutokana na fursa mbalimbali zilizopo kijiografia, kiuchumi na kimazingira, jitihada zinafanyika kupitia Halmashauri na Wadau mbalimbali kuendeleza Halmashauri ya Mji katika nyanja mbalimbali ili kufikia hadhi ya Manispaa siku za usoni.
Mahali:
Halmashauri ya Mji iko umbali wa Kilometa 116 kutoka Makao makuu ya mkoa wa Tabora. Ipo kati ya Latitudo 3°45¢ - 5°00¢ Kusini na Longitudo 32°30¢ - 33°30¢ Mashariki. Halmashauri ya Mji inapakana na Wilaya ya Igunga upande wa mashariki. Upande wa Kaskazini na kusini inapakana na Halmashauri ya Wilaya ya Nzega.
NZEGA TOWN COUNCIL (HALMASHAURI YA MJI NZEGA)
Sanduku la Barua: S.L.P 256 NZEGA-TABORA
Simu ya Mezani: +255677003373
Simu ya Mkononi: +255677003373
Barua Pepe: td@nzegatc.go.tz
Haki miliki zote zimehifadhiwa na nzegatc 2017