WALIMU 184 WA AJIRA MPYA WAPATA MAFUNZO ELEKEZI
Walimu 184 kutoka pande mbali mbali za nchi ya Tanzania walio pata ajira hivi karibu katika Halmashauri mbili yaani Halmashauri ya Mji wa Nzega na Halmashauri ya Wilaya ya Nzega wamepata mafunzo elekezi kuhusu kanuni za maadili na utendaji kazi katika utumishi wa waalimu .
Mafunzo hayo yamefanyika kwenye ukumbi wa Chama Cha Waalimu Wilaya ya Nzega (CWT) siku ya leo tarehe 9 Julai ,2025 ambapo mgeni rasmi alikuwa mkuu wa wilaya ya nzega akiwakilishwa na katibu tawala wa wilaya ya Nzega Bi.Winfreda Funto .
Akifungua mafunzo hayo Bi.Winfreda Funto alianza kwakusema ndugu zangu waalimu mmeingia kwenye utumishi wa rasmi wa serikali ,huku huwa tunatumia sheria na kanuni zinazo tuongoza ukitaka mambo yaende vizuri ishi humo kwenye kanuni hizo na sheria,pia lazima nizamu ya kiutumishi lugha zinazo tumika lazima iwe yakiutumishi .
Mwisho kabisa ndugu zangu waalimu nendeni mkaishi kwa maisha yenu ya uhalisia kwani maisha huenda hatua kwa hatua ,msiende kutamani vitu msivyo viweza ikaja kuwa letea shida alisema .
Leonard Japhet katibu msaidizi tume ya utumishi wa waalimu (TSC)Nzega amewaasa Waalimu hao wahakikishe wanaenda kutoa huduma bora ,japo watakutana na wateja wakorofi wajitahidi kuvumilia pia nendeni mkatunze siri za ofisi nawala kamwe msitoe siri za ofisi kwani wewe ulie toa na ulie pokea hautakuwa salama kabisa .
Nae Juma Ibrahimu Mwalimu mpya wa shule ya Msingi ameishukuru serikali kwakumwajili napia anaona mafunzo hayo yanatija sanaa kwao kwakua wamekaa muda mrefu mtaani hivyo wamekumbushwa alisema .
Mafunzo haya ni miongoni mwajitihada za serikali kuhakikisha watumishi wa umma wanafata sheria na kanuni za utumishi wa Umma
NZEGA TOWN COUNCIL (HALMASHAURI YA MJI NZEGA)
Sanduku la Barua: S.L.P 256 NZEGA-TABORA
Simu ya Mezani: +255677003373
Simu ya Mkononi: +255677003373
Barua Pepe: td@nzegatc.go.tz
Haki miliki zote zimehifadhiwa na nzegatc 2017