KITENGO CHA MICHEZO UTAMADUNI NA SANAA
MAJUKUMU YA KITENGO CHA MICHEZO, UTAMADUNI NA SANAA
Kufundisha fani mbalimbali za michezo
ORODHA YA MALI KALE ZILIZOPO HALMASHAURI YA MJI WA NZEGA
UTANGULIZI:
Halmashauri ya mji Nzega ilipatikana baada ya kugawanywa kwa Halmashauri ya wilaya ya Nzega mwaka 2015 na kuwa na Halmashauri ya mji Nzega ambayo ina ukubwa wa Kilomita za mraba zipatazo 690.57. Kiutawala Halmashauri ya mji imegawanyika katika Tarafa 1, kata 10, Vijiji/Mitaa 35 na Vitongoji 176. Kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022, Halmashauri ina jumla ya watu 125,193 ambapo wanaume ni 60,097 na wanawake ni 65,096. Aidha Shughuli kubwa za kiuchumi ni kilimo, ufugaji, uvuvi, uchimbaji madini na ujasiriamali.
Makao makuu ya wilaya ya Nzega yalikuwa katika mji wa Nzega wa sasa ambapo mwaka 1942 wilaya ilianzishwa kwa kuwepo kwa Ofisi ya mkuu wa Wilaya, Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji, Ofisi za Elimu, Posta, Mawasiliano na Ujenzi na Hospitali ya Wilaya.
UONGOZI:
Mwaka 1942 Wilaya ya Nzega ilipoanzishwa ilikuwa na Mkuu wa Wilaya Mwingereza aliyeitwa Pigions. Huyu alitawala hadi mwaka 1948, ndipo akaingia Resky ambaye alitawala kwa muda mfupi kisha akatawala Ramson hadi mwaka 1955, na mwisho kabla ya Uhuru alitawala Bekker hadi mwaka 1961 wakati wa Uhuru.
Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ilianzia katika jengo la ofisi ambayo kwa sasa ni Ofisi ya mradi wa kilimo baada ya idara ya Elimu msingi kuhamia Ipazi, baadae ofisi hiyo ilihamia mahali ilipo sasa, wakati wa uongozi wa Mkuu wa Wilaya aliyeitwa F. M. Ruangisa mwaka 1979.
OFISI YA MKUU WA WILAYA ENZI ZA UKOLONI
Ofisi ya Mkuu wa Wilaya kabla ya Uhuru. Kwa sasa ni ofisi ya mradi wa kilimo cha mkonge baada ya Idara ya Elimu kuhamia ipazi.
NZEGA TOWN COUNCIL (HALMASHAURI YA MJI NZEGA)
Sanduku la Barua: S.L.P 256 NZEGA-TABORA
Simu ya Mezani: +255677003373
Simu ya Mkononi: +255677003373
Barua Pepe: td@nzegatc.go.tz
Haki miliki zote zimehifadhiwa na nzegatc 2017