KILIMO, MIFUGO NA UVUVI.
Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi ni miongoni mwa Divisheni zinazotoa huduma katika jamii. Divisheni hii inatoa ushauri, elimu na mafunzo kuhusu kanuni za Kilimo, ufugaji na uvuvi bora kwa lengo la kuiwezesha jamii kupata tija katika uzalishaji wa mazao ili kuhakikisha kila kaya inajitosheleza kwa chakula, inaongeza kipato hivyo kupunguza umaskini katika jamii.
Zaidi ya asilimia 70 ya wakazi wa Halmashauri ya Mji wa Nzega hujishughulisha na kilimo na ufugaji. Mazao muhimu ya chakula ni pamoja na Mpunga, Mahindi, Viazi vitamu na Mihogo. Hata hivyo mpunga huzalishwa kama zao la chakula na biashara. Mazao ya biashara ni Pamba Alizeti, korosho na Karanga.
Sekta ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi inachangia zaidi ya 30% katika pato la Halimashauri ya Mji wa Nzega.
MAJUKUMU YA SEKTA YA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI.
Kutoa elimu/mafunzo ya kanuni bora za kilimo, ufugaji na uvuvi kwa njia mbalimbali ikiwemo mihadhara, mijadala, mashamba darasa na mashamba ya mfano.
Kudhibiti visumbufu vya mazao na mimea na mifugo.
Kuhakikisha usalama wa chakula na lishe bora unakuwepo katika ngazi ya kaya kwa kuwashauri wananchi kuhifadhi chakula katika kaya.
Kutoa mafunzo ya matumizi bora ya ardhi kwenye maeneo ya kilimo kwa kupanga na kugawa matumizi ya ardhi kwa shughuli mbalimbali ikiwemo kuongeza uzalishaji tija.
Kutoa taarifa mbalimbali zinazohusu sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi mfano ni wapi pembejeo zinapatikana, hali ya masoko, uwezesho wa kifedha na hata wadau/mashirika yanayowasaidia wakulima,wafugaji na wavuvi kupata mahitaji yao mbalimbali.
Kuwahamasisha wakulima kulima mazao ya biashara ili kuongeza kipato. Kufanya maonesho mbalimbali kupitia siku za wakulima, na hata ngazi ya wilaya kupitia maonesho ya nanenane.
Kutoa mafunzo ya hifadhi ya mazao ya kilimo kwa kuzingatia viwango vinavyohitajika na matumizi sahihi ya viuatilifu vya mazao ya kilimo ghalani.
Kuwatembelea wakulima, wafugaji na wavuvi kwa lengo la kushauri/kutatua changamoto mbalimbali wanazokutana.
Kutoa tuzo na zawadi mbalimbali kwa wakulima, wafugaji na wavuvi ili kuwahamasisha wengine kufuata kanuni bora za kilimo, ufugaji na uvuvi.
Kuboresha miundo mbinu ya Mifugo na Samaki.
Kuboresha miundo mbinu ya umwagiliaji.
NZEGA TOWN COUNCIL (HALMASHAURI YA MJI NZEGA)
Sanduku la Barua: S.L.P 256 NZEGA-TABORA
Simu ya Mezani: +255677003373
Simu ya Mkononi: +255677003373
Barua Pepe: td@nzegatc.go.tz
Haki miliki zote zimehifadhiwa na nzegatc 2017