Idara ya Ardhi na Maliasili
Sekta ya Ardhi na Mipango Miji
Wakazi wa Halmashauri ya Mji wa Nzega wanaishi kwenye maeneo ya makazi yaliyopangwa na kwa sehemu ndogo wanaishi kwenye maeneeo ya makazi holela yasiyo na huduma muhimu na bila uhakika wa haki zao za ardhi. Ili kurekebisha hali hii, kuanzia mwaka 2015 mkakati wa upimaji ulianza na baadhi ya maeneo yamepimwa na elimu inazidi kutolewa ili wananchi kujua umuhimu wa kuishi kwenye maeneo yanayotambulika kisheria.
Katika mwaka wa fedha 2016/2017 imejiwekea lengo la kupanga na kusimamia maendeleo ya makazi. Halmashauri inaendelea na kazi kubwa ya kuandaa michoro ya mipango miji(Detailed planning scheme ili uendelezaji wa ardhi ufanyike kwa kufuata mipango hiyo ya matumizi bora ya ardhi. Jumla ya 100,000,000 zimetengwa kwa ajili ya fidia ya viwanja 600 vinavyotarajiwa kupimwa na kuendelezwa kadiri ya uwezo wa rasilimali fedha utakavyoongezeka.
Upimaji wa Vijiji.
Katika upimaji wa vijiji wa mwaka 2008; vijiji vyote 21 havijapimwa kwani Halmashauri hii ilianzishwa rasmi Julai 2015, hadi kufikia sasa vijiji hivi vinahitaji kufanyiwa upimaji.
Vijiji vilivyo na Mipango ya Ardhi.
Hakuna Vijiji vilivyo na Mipango ya matumizi bora ya Ardhi (Land Use Plan) na mpango utaanza kutekelezwa fedha itakapopatikana ili kutenga maeneo ya makazi, kilimo, ufugaji michezo na maeneo ya hifadhi
Sekta ya Maliasili na Hifadhi ya Mazingira.
MALIASILI
Halmashauri ya mji wa Nzega ina utajiri mkubwa wa maliasili ikiwa ni pamoja na misitu miwiwli ya Kagonho uliopo kata ya Mwanzoli na misitu ya Mwakulu uliopo kijiji cha Kitengwe kata ya Mwanzoli.Misitu hii yote kwa pamoja ina ukubwa wa hekta 3,984.
Vizuizi vya Mazao ya Maliasili na Mazao Mchanganyiko
Katika kudhibiti usafirishaji wa mazao mchanganyiko yasiyolipiwa ushuru na mazao ya Maliasili, Halmashauri ilianzisha kizuizi katika eneo la Itilo (Barabara Kuu), Tabora Mwanza.Kizuizi hiki kinasaidia vile vile katika kuboresha mapato ya Halmashauri.
NZEGA TOWN COUNCIL (HALMASHAURI YA MJI NZEGA)
Sanduku la Barua: S.L.P 256 NZEGA-TABORA
Simu ya Mezani: +255677003373
Simu ya Mkononi: +255677003373
Barua Pepe: td@nzegatc.go.tz
Haki miliki zote zimehifadhiwa na nzegatc 2017