Elimu ya Awali na Elimu Msingi
Majukumu ya idara ya Elimu ya Awali na Elimu Msingi.
(i)Kupanga upatikanaji, usambazaji na matumizi ya rasilimali katika shule za msingi
(ii) Kusimamia upimaji endelevu kwa wanafunzi wa shule za msingi.
(iii) Kusimamia utoaji wa elimu ya watu wazima na elimu nje ya mfumo rasmi katika shule za awali na msingi
(iv) Kuratibu elimu ya stadi za maisha katika shule za msingi.
(v) Kufanya tathmini ya mahitaji ya elimu ya watu wazima na elimu nje ya mfumo rasmi
(vi) Kufuatilia utekelezaji wa mipango na programu za elimu ya awali na msingi
(vii) Kuunda na kutunza hifadhi data ya elimu ya awali na msingi
(viii) Kuratibu na kusimamia shughuli za michezo katika shule za msingi.
Taaluma
Kitengo kitafanya shughuli zifuatazo:-
(i) Kuratibu utekelezaji wa sera, mipango ya elimu ya Awali na Msingi,
duru, na miongozo katika ngazi ya shule
(ii) Kuratibu na kusimamia usimamizi wa upimaji endelevu wa shule na
mitihani ya taifa ya darasa la nne na la saba
(iii) Kufuatilia na kutathmini utekelezaji wa elimu ya awali na msingi
(iv) Kuandaa taarifa za utekelezaji wa mipango na programu za maendeleo ya elimu
(v) Kuratibu utoaji wa elimu kwa ajili ya kujitegemea na kusimamia mapato,
kuzalisha shughuli/mradi katika shule za Msingi.
Vifaa na Takwimu
Kitengo kitafanya shughuli zifuatazo:-
(i) Kukusanya, kuchambua na kutafsiri takwimu za elimu ya Awali na Msingi
(ii) Kuratibu upatikanaji, usambazaji na matumizi ya rasilimali za elimu katika shule za msingi
(iii) Kuratibu takwimu za uandikishaji na vifaa kwa shule
(iv) Kuandaa taarifa za utekelezaji wa maendeleo ya elimu
(v) Kubainisha mahitaji ya rasilimali kwa shule za Halmashauri
Elimu maalum
Kitengo kitafanya shughuli zifuatazo:-
(i) Kuandaa na kusimamia mipango ya utekelezaji wa elimu ya mahitaji maalum kwa shule za msingi
(ii) Kutambua watoto wenye mahitaji maalum na kuwapeleka shule
(iii) Kukusanya taarifa za wanafunzi wenye mahitaji maalum na kushauri ipasavyo
(iv) Kuratibu upatikanaji, usambazaji na matumizi ya rasilimali kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum.
Elimu ya Watu Wazima na na Elimu Nje ya Mfumo Rasmi
Kitengo kitafanya shughuli zifuatazo: -
Taarifa ya idadi ya shule.
Halmashauri ya Mji Nzega ina jumla ya shule 45 zikiwemo shule za serikali 37 na shule zisizo za Serikali 8.
Taarifa za Matokeo kwa mwaka 2024
Katika kipindi cha mwaka 2024, Halmashauri imefanikiwa kuendesha mitihani ya Kuhitimu darasa la saba (PSLE) na mitihani ya upimaji darasa la nne kitaifa (SFNA).
Aidha katika mitihani hiyo, Halmashauri ilifanikiwa kupata ufaulu mzuri kama inavyoonekana katika jedwali A na B hapa chini;
Jedwali A: Matokeo ya mtihani wa kuhitimu darasa la saba (PSLE) 2024.
WALIOSAJILIWA KUFANYA MTIHANI
|
WALIOFANYA MTIHANI
|
WASIOFANYA MTIHANI
|
WALIOFAULU
|
% YA UFAULU
|
||||||||
WAV
|
WAS
|
JML
|
WAV
|
WAS
|
JML
|
WAV
|
WAS
|
JML
|
WAV
|
WAS
|
JML
|
89.19
|
1019
|
1423
|
2442
|
970
|
1371
|
2341
|
49
|
52
|
101
|
870
|
1218
|
2088
|
Jedwali B: Matokeo ya mtihani wa upimaji kitaifa darasa la nne (SFNA) 2024
WALIOSAJILIWA KUFANYA MTIHANI
|
WALIOFANYA MTIHANI
|
WASIOFANYA MTIHANI
|
WALIOFAULU
|
% YA UFAULU
|
||||||||
WAV
|
WAS
|
JML
|
WAV
|
WAS
|
JML
|
WAV
|
WAS
|
JML
|
WAV
|
WAS
|
JML
|
87.4
|
1699
|
1883
|
3582
|
1567
|
1805
|
3372
|
132
|
78
|
210
|
1304
|
1643
|
2947
|
NZEGA TOWN COUNCIL (HALMASHAURI YA MJI NZEGA)
Sanduku la Barua: S.L.P 256 NZEGA-TABORA
Simu ya Mezani: +255677003373
Simu ya Mkononi: +255677003373
Barua Pepe: td@nzegatc.go.tz
Haki miliki zote zimehifadhiwa na nzegatc 2017