TREKTA 20, POWER TILLER KULETA MAPINDUZI YA KILIMO NZEGA MJI
Serikali imeendelea kuthibitisha kwa vitendo nia njema ya kuwainua Wakulima kwa kuhakikisha kuwa vitendea kazi, mbolea na pembejeo zinapatikana kwa urahisi na ukaribu wa Wakulima.
Halmashauri ya Mji Nzega kwa mara ya kwanza katika historia, imepokea na kukabidhiwa trekta 10 combined Harvester moja kutoka Wizara ya Kilimo. Trekta nyingine 10, majembe ya trekta 10 haro 10 na power tillar 9 zimeshawasili kutoka ASA na zimekabidhiwa tayari .
Ujio wa Trekta hizo ni sehemu ya Mipango mikakati ya Dkt Samia Suluhu Hassan, ikisimamiwa kwa umadhubuti mkubwa na Waziri wa Kilimo, Mhe Hussein Bashe kuimarisha usalama wa chakula na kukuza mapato ya Wakulima.
Wakulima wamekuwa wakipewa mafunzo ya mara kwa mara ya kilimo cha kisasa na kanuni bora za kilimo ili kuongeza uvunaji. Mwaka wa fedha 2024/2025, Halmashauri ya Mji Nzega ilitoa mafunzo hayo kwa Wakulima 26,000 kati ya wakulima 56,000
Pia katika kipindi hicho hicho, tani 260 za mbolea ya Ruzuku ilinunuliwa na Wakulima hao.
Hii ilipelekea uvunaji wa mazao yenye tani zaidi ya 50,000 katika kipindi cha mwaka 2023/2024.
Kuanzishwa kwa Skimu ya Umwagiliaji ya Idudumo, kuliwezesha kulimwa kwa hekta 300 kwenye skimu hiyo na kuzalisha tani 1,200 ya Mazao katika msimu wa mwaka 2023/2024. Hii ni kutekeleza kwa vitendo kauli za Dkt Samia Suluhu Hassan za kuhakikisha Wakulima Wanapata tija ya kazi ya
NZEGA TOWN COUNCIL (HALMASHAURI YA MJI NZEGA)
Sanduku la Barua: S.L.P 256 NZEGA-TABORA
Simu ya Mezani: +255677003373
Simu ya Mkononi: +255677003373
Barua Pepe: td@nzegatc.go.tz
Haki miliki zote zimehifadhiwa na nzegatc 2017