Mifugo na Uvuvi ni shughuli inayofanywa na wakazi wengi wa Halmashauri ya Mji Nzega.
Majukumu ya Idara ya Mifugo na Uvuvi/Huduma zinazopatikana katika Idara.
Miundombinu ya Mifugo:
Majosho: Halmashauri ina jumla ya majosho 7 katika Kata za Miguwa,NzegaNdogo,Itilo,NzegamjiniMashagharibi,Uchama,Mbogwe,Uchama.
Machinjio: Kwa sasa Halmashauri ina machinjio moja katika kata ya Nzega mjini magharibi
Minada ya Mifugo: Kuna mnada mmoja wa awali wa Ushirika katika Kata ya Nzega Mjini Magharibi shughuli za biashara ya mnada wa mifugo zinaendelea kwa kila siku ya jumamosi.
Mabwawa ya Kunyweshea Mifugo:Halmashauri ya Mji Nzega ina jumla ya mabwawa saba(7)katika kata za Mwanzoli,Ijanija,Itilo,Nzega Mashariki,Mbogwe,Uchama na Nzega ndogo na mabirika matano(5)katika kata za Mbogwe,Ijanija,Uchama,Miguwa,Ijanija.
Pia Halmashauri ya mji Nzega ina miradi inayotekeleza katika Mnada wa Ushirika kama Ujenzi wa pakilio na shushio la Ng’ombe pia Ujenzi wa Vyoo vya kisasa,Banda la kuuzia nyama,Uzio katika mnada wa Ushirika.
Maradhi ya Mifugo:
Magonjwa ya mifugo yanayoathiri mifugo katika Halmashauri ya mji wa Nzega ni yale yaenezwayo na Kupe kama vile Ndigana kali, Ndigana baridi, homa ya Kizunguzungu,kokojoa Damu (Babesiosis). Vilevile kuna magonjwa ya Mlipuko kama vile ugonjwa wa miguu na midomo(foot and MouthDisease),chambavu(BlackQuarter),mapele ngozi (Lumpy skin disease),Homa ya mapafu(CBPP).Pia kwa jamii ya ndege kuna magonjwa kama kuharisha damu,kideri,Ndui na minyoo.
CHANJO YA KUZUIA MAGONJWA YA MIFUGO
Katika suala zima la kuzuia na kujikinga na magonjwa ya mlipuko, Chanjo mbalimbali za mifugo hutolewa na Idara ya Mifugo na Uvuvi ikishirikiana na wananchi husika.
Jitihada za kuzuia kuenea kwa maambukizi mapya ya magonjwa haya ambayo ni homa ya mapafu (CBPP),Chambavu(Black quarter),Miguu na Midomo(FMD)mapele ngozi(Lumpy skin),Kideri(newcastle),ndui ya kuku(Fowl pox)Kichaa cha Mbwa(rabies) zinafanyika kwa kuwahamasisha wafugaji kuchanja Mifugo yao.
Uhamilishaji wa Mifugo
Hakuna shughuli za uhamilishaji zinazofanyika kwa sasa katika halmashuri ya Mji Nzega.
UVUVI
Uvuvi ni mojawapo ya shughuli zinazofanyika katika Halmashauri ya mji wa Nzega kwa kuwa lipo bwawa la Kilimi katika Kata ya Uchama.
Shughuli za uvunaji wa mazao ya Uvuvi katika Halmashauri ya mji Nzega zinafanyika katika Bwawa la Kilimi lililoko katika kata ya Uchama , Samaki wanaopatikana ni Aina ya sato/perege na Kambare (Catfish).
NZEGA TOWN COUNCIL (HALMASHAURI YA MJI NZEGA)
Sanduku la Barua: S.L.P 256 NZEGA-TABORA
Simu ya Mezani: +255677003373
Simu ya Mkononi: +255677003373
Barua Pepe: td@nzegatc.go.tz
Haki miliki zote zimehifadhiwa na nzegatc 2017