Idara ya Ujenzi
Halmashauri inatekeleza maelekezo ya Sera na Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2015 kwa kuendelea kuimarisha na kuunganisha barabara toka makao makuu ya halmashauri na vijiji ili zipitike kwa wakati wote. Pia inahakikisha ujenzi na ukarabati wa majengo mbalimbali unazingatia viwango vinavyokubalika.
Halmashauri ya Mji Nzega kupitia Idara ya ujenzi inatekeleza majukumu yake ya msingi ikiwa pamoja na kufanya matengenezo ya Barabara ya muda maalumu,matengenezo ya kawaida,maeneo korofi na kuratibu shughuri zote za ujenzi katika Halmashauri.Aidha katika kutekeleza hili Halmashauri kwa kushilikiana na serikali kuu ina jumla ya kilometa 206 za mtandao wa barabara kati ya hizo kilometa 12 ni za kimkoa,na 145 ni za Halmashauri
Hadi sasa Halmashauri ya mji wa Nzega, nje ya Barabara za Mikoa na Barabara kuu imekwisha tengeneza urefu wa kilomita 21.1 kwa kiwango cha Changarawe, kilomita 163 ni Barabara za vumbi, na kilomita 1 ni Barabara ya Lami. Aidha, Mtandao huu wa Barabara umekuwa ukifanyiwa matengenezo kila mwaka kutokana na vyanzo mbalimbali vya fedha vya Halmashauri ya Mji na kufanya barabara hizo kupitika katika vipindi vyote vya mwaka kwa 80%.
Aidha katika mwaka 2015/16 Halmashauri kupitia mfuko wa barabara imeidhinishiwa kupatiwa shilingi milioni 435.63 kwa ajili ya kufanya matengeneza yakawaida, ya muda maalum, kuimalisha sehemu korofi na ujenzi wa makaravati na kwamba utekelezaji wa kazi hizo unaendelea
NZEGA TOWN COUNCIL (HALMASHAURI YA MJI NZEGA)
Sanduku la Barua: S.L.P 256 NZEGA-TABORA
Simu ya Mezani: +255677003373
Simu ya Mkononi: +255677003373
Barua Pepe: td@nzegatc.go.tz
Haki miliki zote zimehifadhiwa na nzegatc 2017