• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
NZEGA TOWN COUNCIL
NZEGA TOWN COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Nzega

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
      • Origin
      • Ukubwa wa Eneo
      • Watu wa Eneo Husika
      • Hali ya Hewa
      • Shughuli za Kiuchumi
      • Orodha ya Madiwani
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mkakati
  • Utawala
    • Muundo wa Tasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Fedha na Biashara
      • Mipango Miji, Ardhi na Maliasili
      • Elimu ya Sekondari
      • Elimu ya Msingi
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ujenzi
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Mipango,Takwimu, Usimamizi na Ufuatiliji
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Uchaguzi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Manunuzi
      • Sheria
      • Ufugaji Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio Vya Utalii
    • Ufugaji
    • Kilimo
  • Huduma Mbalimbali
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha wa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Maadili
      • Ukimwi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kukutana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Miongozo
  • Kituo Cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

Maendeleo ya Jamii

  • Idara ya Maendeleo ya Jamii, katika robo hii ya tatu imeweza kufanya shughuli  mbalimbali  za Maendeleo. Tumetoa  Mafunzo kwa wajasiriamali wanawake na vijana, takribani watu wapatao 402. Aidha tumeshiriki katika shughuli mbalimbali za Maendeleo ikiwemo kushiriki kusimamia pamoja na mafunzo kuhusu kuhamasisha wananchi kuchangamkia fursa mbalimbali na kushiriki kwenye shughuli za maendeleo kwa Watendaji wa Kata, Vijiji na Mitaa. Vile vile, tumesajili jumla ya vikundi 32 vya wajasiriamali, kati ya hivyo Vikundi 15 ni vya vijana na vikundi 17 ni vya wanawake.
  • Shughuli zilizofanyika kwa ujumla ni kama ifuatavyo:-
  • Usajili wa vikundi vya ujasiriamali
  • Ufuatiliaji wa Marejesho ya mikopo ya Wanawake na Vijana
  • Kuhamasisha Wananchi kushiriki kwenye Uchumi wa Viwanda
  • Kutoa elimu kwa Watendaji wa Kata, Mitaa na Vijiji kuhusu Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi pamoja na Fursa zilizopo
  • Kutoa mikopo kwa Vikundi vya Vijana na Wanawake
  • Kutoa elimu ya ujasiriamali kwa Wanawake na Vijana
  • Kuhamasisha wana wake na vijana kujiunga na SACCOS.
  •  UTAWALA
  • Idara hii kwa sasa ina jumla ya Watumishi 06 (me 02 na ke 04) watumishi 05 wpo Makao makuu, Mmoja yupo kwenye kata  ya Itilo. Idara ina mapungufu ya watumishi kumi na tatu (13) kutokana na ikama ya idara kuna mapungufu ya watumishi kumi na tatu. Katika upungufu huo watumishi 10 ni kwa ajili ya  kata zote 10 na watumishi 3 ni kwa ajili ya Vitengo idarani.
  • VITENGO
  • Idara ina vitengo sita kama ifuatavyo:-
    • Kitengo cha wanawake
    • Kitengo cha Vijana
    • Kitengo cha UKIMWI
    • Kitengo cha Watoto
    • Kitengo cha Utafiti, Takwimu na ufuatiliaji
    • Kitengo cha uwezeshaji wananchi kiuchumi
  •  
  • KITENGO CHA WANAWAKE
  • Kitengo hiki kinashughulikia masuala yote yahusuyo wanawake kama vile shughuli za ujasiriamali, sherehe, ukatili unaohusu wanawake na maendeleo ya wanawake kwa ujumla. Vile vile mikopo na usajili wa vikundi vya wanawake pamoja na SACCOS ya wanawake.
  • Katika robo hii tumetoa mikopo kwa vikundi 48 vya wanawake kwa jumla ya Tsh. 81,000,000.00 na kusajili vikundi vikundi 17. Vile vile tulifanya mafunzo ujasiriamali na Ushiriki wa Wananchi kwenye shughuli za uchumi wa Viwanda.
  •  
  •  
  • KITENGO CHA VIJANA 
  • Kitengo hiki kinashughulikia masuala yote yahusuyo Vijana kama vile shughuli za ujasiriamali, sherehe,  na maendeleo ya Vijana kwa ujumla. Vile vile mikopo na usajili wa vikundi vya vijana pamoja na SACCOS ya vijana.
  • Katika robo hii tumetoa mikopo kwa vikundi 09 vya vijana kwa jumla ya Tsh. 35,000,000 na kusajili vikundi vikundi 15. Vile vile tulifanya mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana na ushiriki wao kwenye uchumi wa viwanda.
  • KITENGO CHA UKIMWI
  • Kitengo hiki kinashughulikia masuala yote yahusuyo UKIMWI kama vile shughuli za UKIMWI katika Halmashauri (CMAC), shughuli za UKIMWI katika Kata (WMAC) na shughuli za UKIMWI katika vijiji au mitaa (VMAC), Vile vile,  Kitengo kinajishughulisha na kusaidia watoto wanaosoma Sekondari upande wa mahitaji ya wanafunzi pamoja na Ada za wanafunzi wa High school. Robo hii hatukuwa na bajeti ya kusaidia wanafunzi.
  •  
  • KITENGO CHA WATOTO
  • Kitengo hiki kinashughulikia masuala yote yahusuyo watoto kama vile shughuli za watoto, sherehe za watoto, ukatili unaohusu watoto na maendeleo ya watoto kwa ujumla. Vile vile , mabaraza ya watoto yaliyoundwa kila kata kwa ajili ya kulinda haki za watoto.
  • Katika robo hii tumefanya ufuatiliaji wa mabaraza ya watoto katika ngazi za kata.
  •  
  • KITENGO CHA TAKWIMU, UFUATILIAJI NA UTAFITI
  • Kitengo hiki kinajishughulisha na masuala yote ya ufuatiliaji wa miradi yote ya maendeleo, masuala ya walemavu na makundi yote maalum. Pamoja na kukusanya takwimu za makundi hayo, Kitengo kinajishughulisha na utafiti wa makundi hayo.
  • Katika robo hii tumefanya ufuatiliaji wa mashirika yote yasiyo ya kiserikali yanayofanya kazi katika halmashauri ya Mji wa Nzega. Vile vile tumefanikiwa kufanya uhakiki wa mashirika 9 kama wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii ilivyotuagiza.
  •  
  • KITENGO CHA UWEZESHAJI WANANCHI KIUCHUMI
  • Kitengo kinajishughilisha na masuala yote yahusuyo uwezeshaji wananchi kiuchumi. Masuala ya uwezeshaji wananchi kiuchumi yanaweza yakawa ya fursa za elimu ya ujasiriamali, fursa za kupata masoko, fursa za maonyesho, fursa za mikopo, fursa za kupata ruzuku kutoka mifuko mbalimbali inayotambulika na Baraza la uwezeshaji wananchi kiuchumi.
  • Katika robo hii, tulitoa elimu ya ujasiriamali na kuwatambulisha wananchi juu ya mifuko inayotoa mitaji, ruzuku, mikopo na elimu ili wananchi waweze kuchangamkia.

Vile vile, Halmashauri ya Mji wa Nzega imefanikiwa kutenga na kutoa fedha kiasi cha Tsh. 116,000,000.00 kwaajili ya kuvikopesha Vikundi vya Wajasiriamali Vijana na Wanawake. Kati ya Fedha hizo Tsh. 81,000,000 zilimetolewa kwa Wanawake na Tsh. 35,000,000 zimetolewa kwa Vijana.

Jedwali 3: linaloonyesha Mikopo iliyotolewa kwa Wanawake marejesho, na Baki ya Deni

Mwaka

Mkopo uliotolewa

Mkopo na riba

Idadi ya Vikundi

Marejesho

Baki ya deni

2015/2016
8,000,000
8,800,000
16
8,524,800
275,200
2016/2017
75,500,000
83,050,000
63
11,277,000
71,77300
2017/2018
81,000,000
89,100,000
48
Bado kuanza
89,100,000

Jedwali 4: linaloonyesha Mikopo iliyotolewa kwa Vijana  na marejesho, na Baki ya Deni

Mwaka

Mkopo uliotolewa

Mkopo na riba

Idadi ya Vikundi

Marejesho

Baki ya deni

2015/2016
2,000,000
2,200,000
4
1,675,000
       445,000






2016/2017
36,000,000
39,000,000
19

8,636,000


30,364,000
2017/2018
35,000,000
38,500,000
9
Bado kuanza
38,500,000

 

  •  CHANGAMOTO
  • Idara inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo:-
  • Ufinyu wa Ofisi kwa kuwa Idara ina chumba kimoja tu kiasi kwamba hata wateja wakifika ofisini inakuwa shida..
  • Kata zote 10 hazina wataalamu wa kada ya maendeleo ya jamii
  • Mahitaji ya mikopo ni mengi sana ukilinganisha na fedha inayotengwa.
  • Ugumu wa Wananchi waliokopeshwa fedha kutorejesha kwa wakati hasa vikundi vya Vijana.

MIKAKATI

  • Kuzisimamia SACCOS ya vijana na wanawake ili kuweza kukidhi mahitaji ya fedha za mikopo
  • Kufanya ufuatiliaji wa marejesho kwa wanaochelewesha kurejesha kwa wakati
  • Kuomba kibali cha kuajiri watumishi wengine wa kada ya maendeleo ya jamii.

 

Halmashauri ya Mji wa Nzega imekuwa ikitenga 5% kwa ajili ya mfuko wa vijana  na 5% kwa ajili ya mfuko wa wanawake kutoka katika mapato yake ya ndani kwa kila mwaka. Halmashauri yetu ina jumla ya vikundi 207 vilivyosajiliwa, kati ya Vikundi hivyo Vikundi 154 ni vya wanawake na Vikundi 53 ni vya vijana

Halmashauri hii ilianza rasmi mwaka 2015, Hivyo kuanza kutoa mikopo kwa Vikundi vya Vijana na Wanawake kuanzia Mwaka 2015/16 na tulieendelea kutoa mikopo hiyo 2016/17 na Mwaka 2017/18 tunaendelea kutoa mikopo.

  • Mwaka 2015/16 kiasi kilichotolewa ni Tsh.10,000,000.00 na tulifanikiwa kuvikopesha vikundi 20. Kati ya fedha hizo, Tsh. 8,000,000 ni kwa ajili ya vikundi 16 vya wanawake na Tsh. 2,000,000 ilikuwa kwa vikundi 4 vya vijana.
  •  Mwaka 2016/17 kiasi kilichotolewa kwa Mfuko wa wanawake na Vijana ni Tsh. 111,500,000.00. Kati ya fedha hizo Tsh.75,500,000 ilikuwa kwa ajili ya Vikundi 63 vya wanawake na Tsh. 36,000,000 kwa ajili ya vikundi 19 vya vijana.
  • Mwaka 2017/18, Halmashauri imetenga Tsh. 154,000,000 kutoka mapato yake ya ndani kwa ajili ya vikundi vya wanawake na vijana watakaoomba na kukidhi vigezo. Hadi sasa kipindi cha Julai hadi Disemba tumekwisha toa Tsh. 100,000,000 kwa ajili ya wanawake na vijana yaani Tsh. 65,000,000 Wanawake na 35,000,000 Vijana
  • MAFANIKIO NA FURSA ZILIZOPO
  • Pamoja na Halmashauri kutenga fedha za mapato yake ya ndani bado imeendelea kuhamasisha makundi hayo ya Vijana na Wanawake kuendelea kuchangamkia fursa za ndani ya Halmashauri na nje pia.
  • Halmashauri imefanikiwa kuhamasisha Uanzishwaji wa SACCOS ya Vijana yenye Jumla ya Wanachama waanzilishi 155. SACCOS hiyo ilianzishwa kwa ajili ya kupanua wigo wa kupata mitaji kutoka Wizara ya kazi na vijana, kukopa toka taasisi za fedha na kujenga tabia na kujiwekea akiba ili baadae kuongeza mtaji kwa kukopa.
  •     Vile vile, Halmashauri imefanikiwa kuanzisha SACCOS ya wanawake kwa lengo lile lile na kupanua wigo wa kuongeza mitaji kwa kukopa toka mfuko wa wanawake wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Wazee na Watoto. Zaidi ya hayo kuwawezesha kukopa toka taasisi za fedha na kujenga tabia ya kujiwekea akiba.
  • Aidha, Halmashauri imekuwa ikiendesha mafunzo ya ujasiriamali kwa makundi ya wanawake na vijana. Kipindi cha robo ya kwanza (Julai – Septemba, 2017) tuliendesha mafunzo ya ujasiriamali kwa vikundi 18 vya wanawake na 12 vya vijana.
  • Pamoja na hayo tumeendelea kutoa mafunzo ya utengenezaji wa bidhaa kwa ubora tukishirikiana na TBS katika kipindi cha robo ya Pili (Oktoba – Disemba).
  • Halmashauri kwa kushirikiana na Wadau SNV tumefanikiwa kutoa mafunzo ya kilimo bora kwa vijana 60 kata ya Mwanzoli. Vile vile kwa kushirikiana na SNV tumefanikiwa kutoa mafunzo ya majiko sanifu kwa vijana 60 kata ya Nzega Ndogo.
  • Halmashauri imefanikiwa kupeleka Vikundi vya vijana na wanawake kwenda chuo cha Nyuki kujifunza ufugaji bora.
  • Halmashauri imefanikiwa kupeleka vikundi mbali mbali kushiriki maonesho ya nane nane Tabora, maonesho ya SIDO Kasulu nk.
  • Mikakati ya Halmashauri kwa Upande wa Uwezeshaji wa Vikundi vya Vijana na Wanawake. Halmashauri inaendelea kuhamasisha wanawake kwa vijana kuanzisha Viwanda vidogo na vya kati ili tuwe na Nzega ya Viwanda.
  •  Halmashauri  ya Mji wa Nzega imefanikiwa kutenga maeneo kwa ajili ya shughuli za vijana. Tumetenga ekari 48.71 katika kijiji cha Kitengwe, kata ya Mwanzoli. Eneo hilo limetengwa ili vijana waweze kulitumia kwa shughuli mbalimbali za kijasiriamali kama vile kilimo, ufugaji, viwanda vidogo nk. Vile vile tumetenga ekari 20 kata ya Uchama na ekari 200 maeneo ya Kata ya Nzega Ndogo kwa shughuli za viwanda na uwekezaji.
  • Tumefanikiwa kukiwezesha kikundi cha Fatilika kuweza kupata eneo la kuchakata ngozi ili watengeneze bidhaa za ngozi na kupata masoko kirahisi. Vile vile kikundi hicho kimeanzisha kiwanda kidogo cha kutengeneza viatu vya ngozi, mikoba na mikanda ya ngozi. Pamoja na kiwanda, kikundi hicho kinatumika kufundisha vijana wengine kuchakata ngozi. Tunaendelea kupokea vijana wanakuja kujifunza kutoka ndani na nje ya Nzega. Hadi sasa kuna vijana takribani 21 wamekwishajifunza toka Nzega. Vijana 4 wamejifunza kutoka Karagwe na tunatarajia vijana 8 watakuja kujifunza kutoka Halmashauri ya Meatu.
  • Vile vile kuna kikundi cha Vijana 6 walikwenda Maswa kujifunza kutengeneza chaki. Kwasasa wamekwisha anzisha kiwanda kidogo cha kutenengeneza chaki.
  • Zaidi ya hayo, Halmashauri yetu imefanikiwa kupata tuzo miongoni mwa Halmashauri 10 bora zilizofanya vizuri katika kuwawezesha wanawake wajasiriamali kati ya Halmashauri 185.

CHANGAMOTO ZILIZOPO

  • Asilimia 10% ya mapato ya ndani haitoshelezi vikundi vyote vinavyohitaji mkopo kwa ujumla
  • Vijana walio wengi hawajitambui kiasi kwamba wanashindwa kuchangamkia fursa.
  • Vijana walio wengi wanashindwa kusimamia miradi yao vizuri kiasi kwamba marejesho ya mikopo yao yanasuasua.
  •      Vijana wengi wanapenda sana kuajiriwa kuliko kujiajiri
  • Vijana wengi wanapenda starehe kuliko kufanya kazi
  • FAIDA YA KUWA NA SACCOS
  • Itasaidia kuwajengea wanavikundi tabia ya kujiwekea akiba
  • Itasaidia kupanua wigo wa kukopa toka taasisi zingine kama wizarani na taasisi za fedha
  • Itawajengea uwezo wanachama wa kuweza kuchagua au kuchaguliwa
  • Inawapa wanachama uwezo wa kusimamia vizuri fedha
  • Itakuwa ni chachu ya kuanzisha viwanda
  • Tunatekeleza Ilani ya CCM ya Mwaka 2015

DAWATI LA UWEZESHAJI WANANCHI KIUCHUMI

Lengo la kuanzishwa kwa dawati la uwezeshaji wananchi kiuchumi ni kuratibu utekelezaji wa shughuli za uwezeshaji wananchi na kuwakutanisha                                    

SHUGHULI ZA UWEZESHAJI ZILIZOFANYIKA

  • Kufanya uzinduzi wa jukwaa la uwezeshaji wanawake kiuchumi, takribani wanawake 250 walihudhuria uzinduzi huo kutoka Kata 10 za Mji wa Nzega pamoja na taasisi na mashirika mbalimbali yanayofanya kazi hapa Nzega kama SIDO, Mabenki, TRA, Taasisi za mikopo na wadau wengine wa maendeleo. mgeni rasmi alikuwa Katibu Tawala Mkoa Dr. Thea Ntara.
  • Kufanya uhamasishaji kwa makundi ya vijana na wanawake kujiunga na SACCOS, kuunda vikundi vya kiuchumi na kuvisajili katika kata 10 za Mji wa Nzega.
  • Kuanzisha SACCOS ya wanawake na kuisajili, mpaka kufikia mwezi Machi, 2018 SACCOS hii ilikuwa na wanachama 330
  • Kuendesha mafunzo ya uzalishaji bidhaa zenye ubora kwa kushirikiana na TBS, vikundi 9 vilishiriki. Vikundi vilielekezwa hatua za kuafa pale wanapohitaji nembo ya ubora wa bidhaa na kwanini ni lazima wazalishe bidhaa zenye viwango vya ubora ili waweze kuwa soko la bidhaa hizo ndani na nje ya nchi na kuongeza uzalishaji kwa kuwa na viwanda vidogo na vya kati, lakini pia kulinda afya ya watumiaji wa bidhaa wanazozalisha.
  • Kushuriki mafunzo ya kutengeneza majiko banifu yaliendeshwa na shirika la CABUIPA kwa ufadhili wa SNV. Vijana 60 kutoka vijiji vya Zogolo na Iyuki walishiriki mafunzo hayo. Lengo la mafunzo ni kuwajengea uwezo wa kujitambua, kujiajiri tunapoelekea Tanzania ya viwanda na kutunza mazingira.
  • Kuendesha mafunzo ya kuwajengea uwezo wanawake na vijana walioko katika vikundi mbalimbali vya kiuchumi na kijamii, kuwaandaa wawe tayari kutumia fursa ya miradi mikubwa ya ujenzi wa bomba la maji ya ziwa viktoria na bomba la mafuta. Hali kadhalika Afisa Ushirika awalijengewa uwezo katika masuala ya uendeshaji na usimamizi wa SACCOS ya Vijana na Wanawake  iliyoanzishwa.
  • Kuendesha mafunzo ya ufugaji bora wa kuku wa nyama na mayai kwa kushirikiana na idara ya mifugo na kampuni ya AKM Glitters. Jumla ya wanavikundi 125 walihudhuria.

Matangazo

  • FOMU YA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA 2021 December 17, 2020
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI ZA MUDA October 01, 2019
  • KOROSHO- ZAO LA KIMKAKATI July 23, 2020
  • MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KIDATO CHA KWANZA HALMASHAURI YA MJI NZEGA December 16, 2022
  • Onesha Yote

Habari Mpya

  • WATENDAJI WA INEC WAASWA KUWA WAADILIFU

    April 29, 2025
  • MKURUGENZI WA MJI WA NZEGA ANAWATAKIA WATUMISHI WOTE NA WAKAZI WA MJI WA NZEGA SIKUKUU NJEMA YA PASAKA

    April 20, 2025
  • WAKUU WA IDARA NA VITENGO WA PATA MAFUNZO YA MFUMO WA IFT-MIS

    April 17, 2025
  • MAKAMU MWENYEKITI WA CHAMA CHA MAPINDUZI AFURAHISHWA NA UTEKELEZAJI WA IRANI ASILIMIA 100%

    April 16, 2025
  • Onesha Yote

Video

JARIDA KITUO CHA AFYA ZOGOLO & BULUNDE SEKONDARI
Video Nyinginezo

Kurasa za Haraka

  • Matukio
  • Matangazo
  • Zabuni

Kurasa zinazofanana

  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Tabora RS
  • TAMISEMI
  • Halmashauri ya Wilaya ya Nzega

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea

writingMasterThesis

Ramani ya Sehemu

Wasiliana Nasi

    NZEGA TOWN COUNCIL (HALMASHAURI YA MJI NZEGA)

    Sanduku la Barua: S.L.P 256 NZEGA-TABORA

    Simu ya Mezani: +255677003373

    Simu ya Mkononi: +255677003373

    Barua Pepe: td@nzegatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Binafsi
    • Mlalamikaji
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma

Haki miliki zote zimehifadhiwa na nzegatc 2017