• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
NZEGA TOWN COUNCIL
NZEGA TOWN COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji wa Nzega

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
      • Origin
      • Ukubwa wa Eneo
      • Watu wa Eneo Husika
      • Hali ya Hewa
      • Shughuli za Kiuchumi
      • Orodha ya Madiwani
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mkakati
  • Utawala
    • Muundo wa Tasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Fedha na Biashara
      • Mipango Miji, Ardhi na Maliasili
      • Elimu ya Sekondari
      • Elimu ya Msingi
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ujenzi
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Mipango,Takwimu, Usimamizi na Ufuatiliji
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Uchaguzi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Manunuzi
      • Sheria
      • Ufugaji Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio Vya Utalii
    • Ufugaji
    • Kilimo
  • Huduma Mbalimbali
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha wa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Maadili
      • Ukimwi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kukutana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Miongozo
  • Kituo Cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

Afya na Ustawi wa Jamii

kwa sasa Idara ya Afya  ina watumishi  49 ambapo watumishi kumi na nne (15) ni CHMT na  COOPTED MEMBERS, wenye kada mbalimbali kama vile madaktari, daktari msaidizi, makatibu wa Afya , afisa ustawi wa jamii, afisa afya,  mfamasia, fundi sanifu maabara, tabibu meno,waganga ,afisa wauguzi wasaidizi,wauguzi , wahudumu wa afya na walinzi, ambapo  watumishi kumi na mbili (12) wako katika kituo cha Afya, watumishi kumi na saba (17) wako katika zahanati  na  watumishi wengine watano (5) wanafanya kazi katika Hospitali ya Wilaya.

Idara ya afya imegawanyika katika sehemu kuu mbili ambazo ni Afya Tiba na Afya kinga ,vyote kwa pamoja vinafanya kazi kwa kushirikiana .

  • Afya Tiba; hutoa huduma ya matibabu pamoja na kutoa elimu ya Afya kwa wateja na wagonjwa wanaofika kwenye vituo vya kutolea huduma za Afya .
  • Afya Kinga;  hutoa elimu ya Afya kwa wananchi  kwa ajili ya kujikinga na maradhi/ magonjwa na ajali mbalimbali zinazoweza kujitokeza  (magonjwa ya milipuko na maafa ) ikiwa ni pamoja na kutoa chanjo kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano(5)  na kina mama wajawazito.

Pia Idara ya afya ina jumla ya vituo 10 vyakutolea huduma za afya  vya serikali na vya binafsi kama ilivyoainishwa kwenye jedwali hapo chini;

S/N
JINA LA KITUO 
AINA YA KITUO
MMILIKI
KATA
1
ZOGOLO
KITUO CHA AFYA
SERIKALI
NZEGA NDOGO
2
MWAISELA
KITUO CHA AFYA
BINAFSI
NZEGA MASHARIKI
3
EDEN
KITUO CHA AFYA
BINAFSI
NZEGA MASHARIKI
4
SAMORA
ZAHANATI
SERIKALI
NZEGA MASHARIKI
5
MBOGWE
ZAHANATI
SERIKALI
MBOGWE
6
MIGUWA
ZAHANATI
SERIKALI
MIGUWA
7
UNDOMO
ZAHANATI
SERIKALI
UCHAMA
8
MASAM
ZAHANATI
BINAFSI
NZEGA MAGHARIBI
9
TUMAINI LA JAMII
KLINIKI
BINAFSI
NZEGA MAGHARIBI
10
FARAJA
KLINIKI
BINAFSI
NZEGA MASHARIKI

SHUGHULI MBALIMBALI ZINAZOFANYIKA KWENYE IDARA/ KITENGO.

Idara ya Afya imeendelea kufanya shughuli mbalimbali za Afya katika vituo vyote vya kutolea huduma za Afya Kama ifuatavyo;

SHUGHULI ZA UTAWALA.

  • Kufanya usimamizi elekezi katika vituo vyote vyakutolea huduma za afya tiba, afya kinga na ustawi wa jamii.
  • Kuandaa taarifa mbalimbali za utekelezaji wa shughuli za maendeleo ya Idara ya Afya.
  • Kusambaza madawa, vifaa tiba , vitendanishi na chanjo katika vituo vya kutolea huduma.
  • Kusimamia shughuli za usafi wa mazingira kwenye kata, vijiji na vitongoji vyote vilivyopo Halmashauri ya Mji.
  • Kuingiza takwimu kwenye mfumo wa taarifa (mtuha) kutoka katika vituo vyote vya kutolea huduma .
  • Kusimamia uwajibikaji na stahiki za watumishi wa idara ya Afya.
  • Kusimamia huduma  kwa wateja na wagonjwa  wanaokuja kupata huduma katika vituo  vya kutolea huduma  za afya.
  • Kuhakikisha na kuisimamia watoto , walemavu na wazee wanapa haki zao za msingi.
  • Kusimamia utumiaji wa miongozo ,sheria na taratibu za kazi kwa watumishi wote wa idara ya afya kwa ujumla.
  • Kusimamia vituo vya kutolea huduma ili viweze kutoa huduma bora za afya,kwa kuwa na stoo zilizo katika viwango na pia kuwa na kumbukumbu nsahihi za madawa na vifaa tiba kwa njia ya mafunzo kazini (On Job training-OJT) na usimamizi shirikishi.

AFYA  YA UZAZI  NA  MTOTO.

Shughuli  zinazofanywa ;

  • Huduma ya uzazi wa mpango [family planning].
  • Huduma kwa mama wajawazito [ANC].
  • Huduma kwa wazazi[Labour and delivery].                   
  • Huduma kwa akinamama   baada ya kujifungua [PNC],
  • Huduma za afya ya watoto,              
  • Huduma ya kuzuia maambukizi toka kwa mama kwenda kwa mtoto [PMTCT],
  • Huduma za afya ya uzazi kwa Vijana,
  • Upatikanaji wa dawa muhimu za kupunguza   vifo vya akinamama vitokanavyo  na uzazi.
  • kuzuia vifo vya watoto umri siku 0-28[neonatal death],umri chini ya miaka mitano [ 5], na vifo vya akinamama vitokanvyo nauzazi [Maternal Death].         
  • katika utoaji wa huduma za afya,k wa afya ya uzazi na mtoto mji tunavyo vituo vya afya vitano [5],    vya kutolea  huduma
  • Vituo vyote vinatoa huduma ya PMTCT [Prevention from Mother to child transmition].

  • SHUGHULI ZA USTAWI WA JAMII.
    Kitengo hiki kina Ofisi iliyopo Hospitali ya Wilaya Nzega. Ofisi  hii inatoa huduma za Usatwi wa Jamii kwa wakazi wa Kata kumi (10) zilizopo katika Halmashauri ya Mji. Aidha Kitengo hiki kinasimamia Makao ya Watoto yatima yanayoitwa Verberg Home of Peace kilichopo maeneo ya Tazengwa,Vituo vinne (4) vya kulelea Watoto Wadogo Mchana ambavyo ni  CHAWATA day care center, KKKT, FPCT na Cross Power. Pia kambi/makao ya Watu wenye Ulemavu yaliyopo Iduguta Kata ya Miguwa.
    Shughuli  zinazofanywa na Ofisi ya Ustawi wa Jamii zimegawanyika           katika vipengele vitatu kama vifuatavyo;
    A; HUDUMA KWA FAMILIA, WATOTO NA MALEZI YA AWALI YA WATOTO. shughuli zinazofanyika sehemu hii ni pamoja na:-
    • Huduma za Usuluhishi wa ndoa zenye mifarakano
    • Huduma ya matunzo kwa watoto walio kwenye ndoa zenye mfarakano
    • Huduma ya matunzo kwa watoto wanaozaliwa nje ya ndoa
    • Huduma katika makao ya kulelea Watoto yatima na walio katika mazingira hatarishi, matunzo na ulinzi toka kwa wazazi/walezi na ndugu kutokana na sababu mbalimbali kama vile kifo, kutelekezwa, n.k
    • Huduma ya malezi, makuzi na maendeleo changamshi ya awali kwa watoto wadogo
    • Huduma kwa familia zenye dhiki.
    •  
  • B. MAREKEBISHO YA TABIA NA HAKI ZA MTOTO KISHERIA.

    Shughuli zinazofanyika sehemu hii ni pamoja na:-

    • Haki za Watoto / Vijana (Juvenile Justice)
    • Huduma katika Mahabusu za Watoto
    • Huduma za shule ya Maadilisho
    • Huduma kwa Watoto Watukutu
    • Huduma zitolewazo katika Mahakama ya Watoto
    • Huduma kwa Watoto wanaoishi mitaani.
  • C. HUDUMA KWA WATU WENYE ULEMAVU NA WAZEE

    Shughuli zinazofanyika sehemu hii ni pamoja na:-

    • Mafunzo ya Stadi za kazi kwa watu wenye Ulemavu;
    • Utengemao kwa Watu wenye Ulemavu.
    • Matunzo kwa watu wenye Ulemavu/Wasiojiweza .
    • Nyenzo za Kujimudu .
    • Huduma kwa Vyama/Asasi za Watu wenye Ulemavu.
  • SHUGHULI  ZA  CHANJO.   

    Taarifa za kiujumla  kitengo cha chanjo  kinashughulika na hutoaji wa huduma zote za watoto chini ya miaka mitano na magonjwa yote ya milipuko yanayotolewa taarifa katika jamii.

    Shughuli  zinazofanyika katika kitengo cha chanjo.

    • Kuhakikisha  dawa za chanjo zinapatikana kutoka mkoani.
    • Kusambaza mitungu ya gase na dawa za chanjo kwenye vituo vitano vya   mji vya  kutolea huduma .
    • Kuandaa   taarifa sahihi za chanjo kwa kutumia mfumo    wa  wizara DVD MT na VIMS.
    • Kuhakikisha watoto wote chini ya miaka mitano  wanapata  chanjo  ambao ni sawa na walengwa  2582 kwa mwaka 2017.
    • Kutoa taarifa  za magonjwa ya kuambukiza yanayotokana na chanjo.
    • Kufanya usimamizi shirikishi kwenye vituo vya kutolea huduma.
  • Huduma zinazotoa.

    • Kuhamasisha jamii kupeleka watoto klinic na akinamama wajawazito kupata chanjo.
    • Kutoa elimu ya afya kwa jamii juu ya umuhimu wa kupeleka watoto klinic.
    • Kutoa taarifa za chanjo kwa watoto chini ya miaka mitano na akina mama wajawazito.
  • DAWA  NA VIFAA TIBA

    Kitendo Cha Madawa kina dhima ya kuhakikisha upatikanaji wa Madawa,Vifaa tiba,Vitendanishi na vifaa vya maabara kwa vituo vya kutolea huduma za afya,ambazo ni zahanati 4 (nne) na Kituo cha afya 1 (kimoja).

    Shughuli ya Kitengo.

    • kutayarisha maoteo ya mahitaji ya mwaka na kuyawasilisha kwa bohari ya madawa.
    • kuoanisha mahitaji hayo dhidi ya vyazo mbalimbali vya fedha ambavyo ni pamoja na Ruzuku toka Wizara ya Afya,Mfuko wa pamoja (Health Sector basket Fund),Fedha toka Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) na ule wa Afya ya Jamii (NHIF) na papo kwa papo.
    • Kuagiza dawa na vifaa tiba toka Bohari ya madawa ya Kanda (Tabora) na kisha kuzisambaza hadi vituoni.
    • Utunzaji wa kumbukumbu za fedha,kumbukumbu za  mali nk
    • Kuhakikisha huduma za Madawa zinazotolewa na wahudumu binafsi (wafanyabiashara) zipo katika viwango stahiki.Hivyo ukaguzi wa maduka ya madawa unafanyika mara kwa mara na kisha kupendekeza yapewe vibali vya kutolea huduma toka kwa baraza la Famasi
    • Ukaguzi wa maduka ya vipodozi na kuielimisha jamii juu ya madhara ya vipodozi vyenye viambata  sumu .
  •  MFUKO WA AFYA YA JAMII (CHF)

    Mfuko huu wa Afya ya Jamii  (CHF) ni kwa ajili ya kurahisisha upatikanaji wa huduma za Afya kwa gharama nafuu unaweza kujiunga kama kaya, mtu binafsi, au vikundi kwa kutoa au kuchangia kiasi cha elfu 10,000/= kwa mwaka kwa watu sita (6) tu. Hivyo mwanakaya atakapoumwa atatakiwa kwenda na kadi hiyo katika kituo cha kutolea huduma kilicho karibu naye ili aweze kupatiwa matibabu.

    Matumizi ya fedha zinazotokana na mfuko huu ni manunuzi ya dawa na vifaa tiba, posho na ukarabati katika kituo kilichoandikisha wanachama. Kadri wanachama wanapokuwa wengi ndiyo upatikanaji wa dawa na vifaa tiba utaongezeka.

    Katika Halmashauri ya Mji kuna vituo vitano (5) ambavyo unaweza kwenda kujiandikisha na wategemezi wako ili kuweza kupatiwa kadi ya matibabu, vituo hivyo ni Zahanati ya Samora, Zahanati ya Miguwa, Zahanati ya Mbogwe, Zahanati ya Undomo na Kituo cha Afya Zogolo

    HUDUMA /SHUGHULI  ZA  MFUMO WA TAARIFA ZA UENDESHAJI WA HUDUMA ZA AFYA (MTUHA).

    • Mfumo wa Taarifa za Uendeshaji wa Huduma za Afya (MTUHA) inafanya mambo yafuatayo;
    • Kuingiza takwimu zinazotoka kwenye vituo vya kutolea huduma za Afya kwenye mfumo wa DHIS2.
    • Kuhakiki takwimu zilizo ingia kwenye mfumo wa DHIS2.
    • Kuchambua ubora wa takwimu zilizokuja kutoka katika vituo vya kutolea huduma.
    • Kupakua taarifa za takwimu kutoka kwenye mfumo wa DHIS2 mara zinapohitajika.
    • Kufuatilia na kusimamia ujazaji wa vitabu vya MTUHA na usambazaji wa vitabu hivyo katika vituo vya kutolea huduma za Afya

Matangazo

  • FOMU YA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA 2021 December 17, 2020
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI ZA MUDA October 01, 2019
  • KOROSHO- ZAO LA KIMKAKATI July 23, 2020
  • MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KIDATO CHA KWANZA HALMASHAURI YA MJI NZEGA December 16, 2022
  • Onesha Yote

Habari Mpya

  • WATENDAJI WA INEC WAASWA KUWA WAADILIFU

    April 29, 2025
  • MKURUGENZI WA MJI WA NZEGA ANAWATAKIA WATUMISHI WOTE NA WAKAZI WA MJI WA NZEGA SIKUKUU NJEMA YA PASAKA

    April 20, 2025
  • WAKUU WA IDARA NA VITENGO WA PATA MAFUNZO YA MFUMO WA IFT-MIS

    April 17, 2025
  • MAKAMU MWENYEKITI WA CHAMA CHA MAPINDUZI AFURAHISHWA NA UTEKELEZAJI WA IRANI ASILIMIA 100%

    April 16, 2025
  • Onesha Yote

Video

JARIDA KITUO CHA AFYA ZOGOLO & BULUNDE SEKONDARI
Video Nyinginezo

Kurasa za Haraka

  • Matukio
  • Matangazo
  • Zabuni

Kurasa zinazofanana

  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Tabora RS
  • TAMISEMI
  • Halmashauri ya Wilaya ya Nzega

World visitors tracker

world map hits counter

Waliotembelea

writingMasterThesis

Ramani ya Sehemu

Wasiliana Nasi

    NZEGA TOWN COUNCIL (HALMASHAURI YA MJI NZEGA)

    Sanduku la Barua: S.L.P 256 NZEGA-TABORA

    Simu ya Mezani: +255677003373

    Simu ya Mkononi: +255677003373

    Barua Pepe: td@nzegatc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Binafsi
    • Mlalamikaji
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma

Haki miliki zote zimehifadhiwa na nzegatc 2017