MKURUGENZI SHOMARY MNDOLWA AWAASA AJIRA MPYA KIJIEPUSHA NA RUSHWA ,ULEVI KWENYE MAENEO YA KAZINI
Kikao cha Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Nzega Ndg.Shomary Salim Mndolwa na Watumishi wa Ajira mpya wa Halmashauri ya Mji Nzega kimefanyika siku ya ijumaa Tarehe 10, Octoba ,2025 kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Mji uliopo eneo la Ipazi.
Lengo la kikao hicho ilikuwa nikuwakumbusha mambo mbalimbali yanayo husu utumishi wa Umma kwa watumishi hao waajira Mpya .
Akizungumza nao Mkurugenzi wa Mji wa Nzega alisema’’najua mmekaa mtaani muda mrefu hivyo kama huna nidhamu hakikisha unakuwa na nidhamu maana huku lazima mtumishi waumma uwe na nidhamu ,pia jiepusheni na rushwa usilewe wakati upo kazini nikikukuta nakuchukulia hatua alisema .
Nae Mkuu wa Divisheni ya Utawala na Rasilimali Watu Bi.Leah Kibaki alipata wasaa wakutoa neno kwa Watumishi hao wapya alisema “Natambua hii kazi mmeitafuta kwa muda mrefu hivyo mmeipata nendeni mkatoe huduma bora kwa Wananchi watakuja wateja waaina tofauti tofauti hivyo wavumilieni ili muiwakilishe serikali vizuri’’ alisema .
Kikao hiki nimiongoni mwa jitihada zinazo fanywa na Mkurugenzi wa Mji wa Nzega kuhakikisha watumishi wa Mji wa Nzega wanapata elimu mbali mbali iliwakaweze kutimiza majukumu yao kikamilifu .
NZEGA TOWN COUNCIL (HALMASHAURI YA MJI NZEGA)
Sanduku la Barua: S.L.P 256 NZEGA-TABORA
Simu ya Mezani: +255677003373
Simu ya Mkononi: +255677003373
Barua Pepe: td@nzegatc.go.tz
Haki miliki zote zimehifadhiwa na nzegatc 2017