Halmashauri ya Mji wa Nzega, iliyoko katika Mkoa wa Tabora, ilianzishwa rasmi tarehe 12 Septemba 2014. Kabla ya hapo, eneo hili lilikuwa sehemu ya Halmashauri ya Wilaya ya Nzega. Mji wa Nzega ulipata hadhi ya kuwa mamlaka ya Mji Mdogo kutokana na kasi yake ya ukuaji, na hatimaye kuwa Halmashauri ya Mji.
Halmashauri hii inapatikana katika latitude 3°45-5°00 upande wa kusini mwa mstari wa Ikweta na longitudo 32°30-33°30 Mashariki mwa mstari wa Greenwich,Mji wa Nzega hupata mvua kati ya Milimita 650 mpaka milimita 1200 kwa Mwaka ,Joto huwa linafikia 28°c-30°c na mwezi wa Oktoba hutarajiwa kuwa na joto la hali ya juu .
Halmashauri hii inajumuisha mchanganyiko wa makabila mbalimbali, yakiwemo Wasukuma, Wanyamwezi, Waha, na Wanyiramba, huku Wanyamwezi wa kiwa ndio wenyeji wa eneo hili. Nzega iko umbali wa kilomita 116 kutoka makao makuu ya Mkoa wa Tabora, na inapakana na Wilaya ya Igunga upande wa mashariki, na Halmashauri ya Wilaya ya Nzega upande wa kaskazini , kusini na Magharibi.
Kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2022, Halmashauri ya Mji wa Nzega ilikuwa na wakazi wapatao 125,193.
Kutokana na fursa mbalimbali zilizopo kijiografia, kiuchumi, na kimazingira, jitihada zinaendelea kufanywa na Halmashauri pamoja na wadau mbalimbali ili kuendeleza mji huu katika nyanja mbalimbali, kwa lengo la kufikia hadhi ya Manispaa katika siku za uson
NZEGA TOWN COUNCIL (HALMASHAURI YA MJI NZEGA)
Sanduku la Barua: S.L.P 256 NZEGA-TABORA
Simu ya Mezani: +255677003373
Simu ya Mkononi: +255677003373
Barua Pepe: td@nzegatc.go.tz
Haki miliki zote zimehifadhiwa na nzegatc 2017