Halmashauri ya mji Nzega ilianza kulima korosho katika msimu wa kilimo 2017/2018.Mpaka sasa tumelinda zaidi ya ekari 75 zilizolimwa korosho na jumla ya mikorosho 2,502
Hivi karibuni mafunzo ya kilimo cha korosho yalitolewa na watafiti wa kilimo toka kituo cha utafiti (TARI) Naliendere kwa Wataalam wa Kilimo na Wakulima wa zao hilo.Mafunzo hayo yalikuwa na lengo la kuwajengea wataalam wa Kilimo na Wakulima wa zao hilo ili waweze kuzalisha zao hili kwa tija na hatimaye waongeze kipato cha kaya na Taifa kwa ujumla.
Mada zilizofundishwa ni :Agronomia ya korosho,kuandaa shamba,jinsi ya kutambua na kukinga/kuzuia wadudu waharibifu wa zao la korosho,jinsi ya kutambua magonjwa mbalimbali ya korosho na namna ya kutibu, jinsi ya kuchanganya viwatilifu na kupuliza katika shamba la korosho na kupogolea mikorosho (pruning)
Awali akifungua mafunzo hayo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji aliwasisitiza Wataalam na Wakulima kuwa mafunzo hayo ni muhimu sana kwani Serikali chini ya Mh.Rais Dr John Pombe Magufuli imedhamiria kuinua hali ya wakulima wa zao la korosho lakini pia kufanya zao la korosho kuwa ni moja zao la kimkakati la Kitaifa.
Aliwashukuru pia Watafiti hao kwa kutoa mafunzo kwa Wakulima pamoja na Wataalam
NZEGA TOWN COUNCIL (HALMASHAURI YA MJI NZEGA)
Sanduku la Barua: S.L.P 256 NZEGA-TABORA
Simu ya Mezani: +255677003373
Simu ya Mkononi: +255677003373
Barua Pepe: td@nzegatc.go.tz
Haki miliki zote zimehifadhiwa na nzegatc 2017