VIONGOZI KUTOKA OFISI YA RAIS TUME YA UTUMISHI WA UMMA WAZUNGUMZA NA CMT
Watumishi kutoka Ofisi ya Rais tume ya utumishi wa umma wamefanya kikao kifupi na timu ya uongozi ya Halmashauri ya Mji wa Nzega (CMT).
kikao hicho kimeongozwa na Bi.Terewael R.Foya Mkaguzi kiongozi kutoka Ofisi ya Rais Tume ya Utumishi wa Umma wakishirikiana na Bi.Salome A.Mhekela .
lengo la kikao hicho nikueleza madhumuni yakuja hapo kwenye ofisi ya Halmshauri ya Mji wa Nzega kuja kufanya ukaguzi wakawaidi wa siku zote.
Bi Terewael R.Foya ameleza maeneo yatakayo kaguliwa na pia kuomba ushirikiano kwa Timu hiyo ya Uongozi .
Nae Bi.Leah Kibaki akimuwakilisha Mkurugenzi wa Mji wa Nzega Ndg.Shomary Mndolwa amesema sisi tupo tayari kwa ukaguzi na kwamba tutatoa ushirikiano wakutosha kwenu alisema.
Ukaguzi huo utachukua siku nne kuanzi leo siku ya Ijumaa na utahitimishwa siku ya jumatatu
NZEGA TOWN COUNCIL (HALMASHAURI YA MJI NZEGA)
Sanduku la Barua: S.L.P 256 NZEGA-TABORA
Simu ya Mezani: +255677003373
Simu ya Mkononi: +255677003373
Barua Pepe: td@nzegatc.go.tz
Haki miliki zote zimehifadhiwa na nzegatc 2017