Mganga Mkuu wa Halmashuri ya Mji Dr Jabil Juma amefunga mafunzo ya Mfuko wa afya ya jamii (CHF) iliyoboreshwa yaliyofanyika katika ukumbi wa Ashock kwa siku tatu toka tarehe 07/05/2018 hadi 09/05/2018 washiriki wakiwa ni watoa huduma za afya wawili na wanakamati wawili kutoka kila Zahanati na kila Kituo cha afya.
Mada kuu katika mafunzo hayo yalikwa ni pamoja na:
Mafunzo hayo yaliendeshwa na Wataalam wa Halmashauri wailopata mafunzo juu ya mfumo huo ambao ni:
Mafunzo mengine yataendelea kwa maafisa waandikishaji (Enrollment Officer) watakaochaguliwa kutoka kila mtaa/kijiji ambao kazi yao kubwa ni kuwaandikisha wanachama wa CHF kwa ada ya 30,000/= kwa kaya.
Dr Jabil aliwata washiriki waliopata mafunzo kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao ipasavyo na kwamba hataacha kuwachukulia hatua watakaoshindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo.Amewataka pia kuhakikisha wanakuwa na takwimu sahihi kwani kotukuwa na takwimu sahihi kunasababishia Halmashauri kukosa fursa mbalimbali zinazotokana na kuwa na takwimu na takwimu sahihi.
Aidha aliwasihi wanakamati walioshiriki katika mafunzo hayo kuhakikisha wanafanya uhamisishaji kwa jamii ili kujiunga na mfuko wa jamii ya Afya NHF iliyoboreshwa ikiwa ni moja ya majukumu yao.
NZEGA TOWN COUNCIL (HALMASHAURI YA MJI NZEGA)
Sanduku la Barua: S.L.P 256 NZEGA-TABORA
Simu ya Mezani: +255677003373
Simu ya Mkononi: +255677003373
Barua Pepe: td@nzegatc.go.tz
Haki miliki zote zimehifadhiwa na nzegatc 2017