Waziri wa Habari ,Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe, amefungua Kikao kazi cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini kinachofanyika katika ukumbi wa AICC Mkoani Arusha.Kikao hicho kitafanyika kuazia tarehe 12 Machi 2018 hadi 16 Machi 20018 ikwa na lengo la kuwanoa/kuwawezesha Maafisa Mawasiliano katika kutekeleza majukumu yao ya kutangaza utekelezaji wa ahadi za Serikali ya awamu ya tano.
Kauli mbiu ya kikao kazi hicho ni “Je, Mawasiliano ya Kimkakati Yanachagiza Vipi Tanzania ya Viwanda?”
Akifungua kikao hicho Dkt. Mwakyembe alisema kuwa nchi imedhamiria kuwa Nchi ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025. Hivyo ni kazi ya Maafisa Habari kupeleka habari kwa wananchi juu ya shughuli mbalimbali zinazofanywa na Serikali.Utoaji wa habari kwa Wananchi sio utashi tena bali sheria inasisitiza hilo.Serikali inatarajia Mafisa Habari kuwa wabunifu na kuhakikisha wananchi wanapata haki yao ya kupata taarifa sahihi kwa wakati kuhusu Serikali yao.
NZEGA TOWN COUNCIL (HALMASHAURI YA MJI NZEGA)
Sanduku la Barua: S.L.P 256 NZEGA-TABORA
Simu ya Mezani: +255677003373
Simu ya Mkononi: +255677003373
Barua Pepe: td@nzegatc.go.tz
Haki miliki zote zimehifadhiwa na nzegatc 2017