Kwa kuzingatia umuhimu na mchango unaotolewa na Watendaji Kata na Maafisa Ugani , Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Nzega amegawa pikipiki kumi na tisa (19) kwa lengo la kuwajengea uwezo na kurahisisha utendaji kazi kwa maafisa hawa kwani wao ndo wako karibu na wananchi.
Akimkaribisha mgeni rasmi, Dr Jasper kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Nzega alieleza kuwa lengo kuu la kuwapatia pikipiki Maafisa hawa ni kuwajengea uwezo na kuwarahisishia kazi ili waweze kuwafikia kwa urahisi wananchi na kuwapa huduma kwa wakati.
Akikabidhi pikipiki hizo, Mgeni rasmi ACP Advera Burimba ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Nzega alimpongeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Nzega ndugu Philemon Magesa na kusema kuwa kitendo alichokifanya ni mfano ambao unafaa kuigwa na Wakurugenzi wengine wa Halmashauri za Mkoa wa Tabora.
Mgeni rasmi aliwasisitiza maafisa waliopatiwa Pikipiki hizi kuzitumia kwa malengo yaliyokusudiwa na kuongeza kuwa Uongozi hautasita kumnyang’anya yeyote atakayetumia vyombo hivi kinyume na malengo yaliyokusudiwa.
Pia aliwaasa maafisa hao kuzingatia kanuni, taratibu na sheria za barabarani wakati wa matumizi ya vyombo hivi ili kulinda usalama wao na wa wengine
NZEGA TOWN COUNCIL (HALMASHAURI YA MJI NZEGA)
Sanduku la Barua: S.L.P 256 NZEGA-TABORA
Simu ya Mezani: +255677003373
Simu ya Mkononi: +255677003373
Barua Pepe: td@nzegatc.go.tz
Haki miliki zote zimehifadhiwa na nzegatc 2017