HALMASHAURI ya Mji wa Nzega imefanikiwa kuvuka lengo la makusanyo lilowekwa na Serikali Kuu ambapo kila Halmashauri inatakiwa kutopungua asilimia 80 ya makisio lakini Halmashauri imefikisha asilimia 98.3 ya makisio yake.
Kauli hiyo ilitolewa na Mwenyekiti wa Halmashauri William Jomanga wakati wa Mkutano wa robo ya nne wa Baraza la Madiwani lililofaanyika tarehe 31.07.2018
Alisema kuwa kabla ya kodi ya majengo, kodi ya ardhi Na ushuru ya mabango kuondolewa kwenye mapato ya ndani ya Halmashauri na kupelekwa Serikali kuu walikisia kufikia makusanyo ya biloni 1.63.
Jomanga alisema baada ya vyanzo kuondolewa lengo lilishuka na kubaki kiasi bilioni 1.45 na kuongeza kuwa hatua hiyo inatokana na kuondolewa milioni 177 katika makisio yake ya awali.
Alisema hadi kufikia mwisho wa mwaka wa fedha uliopita Halmashauri ilifanikiwa kukusanya shilingi 1.43 sawa na asilimia 98.3.
Kwa upande wa Mkuu wa wilaya ya Nzega Godfrey Ngupula aliipongeza Halmashauri kwa kufanya vizuri katika kuhakikisha wanavuka lengo liliagizwa na viongozi wa Kitaifa la asilimia 80.
Aliwataka wasibweteke bali waongeze bidii katika kukusanya mapato ikiwemo kuwatoza faini wanaotupa takataka ovyo mitaani na wale wa kwenye mabasi ambayo abiria wake wana tabia ya kutupa taka barabarani kwa sababu ya kukosa vifaa vya kuweka taka ndani ya gari zao.
Ngupula aliongeza kuwa pia wanatakiwa kuhakikisha wanawaondoa Madalali katika vibanda 500 vinavyomilikiwa na Halmashauri hiyo ili waweze kukusanya kodi kuliko ilivyo hivi sasa ambapo hawapati fedha yoyote zaidi ya ushuru wakati vibanda ni vyao.
Alisema wapangaji wanatakiwa waiingie mkataba wa upangaji na Halmashauri na sio Madalali ambao wamekuwa wakiwanyonyaji kuwatoza kodi ya pango kubwa.
Kwa upande wa Katibu Tawala Msaidizi kwa upande wa Serikali za Mitaa Mkoa wa Tabora Nathalis Linuma aliwataka Madiwani na Watendaji wa Halmashauri kuendelea kubuni vyanzo vipya vya mapato kwa ajili ya kujiwekea mazingira mazuri ya kuelekea kujitegemea kwa asilimia 100 ifikapo mwaka 2025.
NZEGA TOWN COUNCIL (HALMASHAURI YA MJI NZEGA)
Sanduku la Barua: S.L.P 256 NZEGA-TABORA
Simu ya Mezani: +255677003373
Simu ya Mkononi: +255677003373
Barua Pepe: td@nzegatc.go.tz
Haki miliki zote zimehifadhiwa na nzegatc 2017