Zoezi la uoteshaji wa miche ya miti aina ya midodoma likiendelea katika kitalu cha Halmashauri ya Mji Nzega ikiwa na maandalizi ya kampeni ya upandaji miti kwa msimu ujao wa 2018/2019.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Ndg.Philemon M. Magesa amelenga kuzalisha miche ya miti 125,000 kwaajili ya msimu ujao. Hadi sasa tayari miche 120,000 iko tayari kwaajili ya kupandikiza kwenye viriba zoezi linaloendelea kwa sasa.Mkurugenzi amesema kuwa baada ya zoezi la kuhamishia miche kwenye viriba kumalizika kila kata itagawiwa jumla ya miche 10,000 kwaajili ya kukuza na kutunza ambapo itapandwa katika kata husika.
Aidha Mkuu wa Idara ya Mipango Miji Ardhi na Maliasili Ndg. John D. Rikanga alieleza kuwa miti hiyo pamoja na kugawiwa kwa kila Kata pia taasisi za Serikali na zisizo za Serikali na taasisi za Dini zitagawiwa miche hiyo.Lengo ni kila mmoja ashiriki katika zoezi zima la utunzaji wa mazingira kwa kupanda miti katika maeneo yao.
NZEGA TOWN COUNCIL (HALMASHAURI YA MJI NZEGA)
Sanduku la Barua: S.L.P 256 NZEGA-TABORA
Simu ya Mezani: +255677003373
Simu ya Mkononi: +255677003373
Barua Pepe: td@nzegatc.go.tz
Haki miliki zote zimehifadhiwa na nzegatc 2017