Na James Kamala, Afisa Habari – Halmashauri Ya Mji Nzega
Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Nzega imepokea gari la kubeba wagonjwa wa dharura (ambulace) ili kuwawaisha kwenye huduma za matibabu ya haraka wagonjwa wanaosumbuliwa na maradhi mbalimbali na wakazi wa mji huo kwa ujumla.
Hili ni gari la pili la aina hiyo kutolewa na serikali ndani ya kipindi cha miezi sita ili kurahisisha huduma za afya kwa wangonjwa wa dharara. Gari lingine la aina hiyo lilitolewa hivi karibuni na kuanza kazi rasmi mwezi januari mwaka huu.
Akitoa taarifa wakati wa makabidhiano ya gari hilo aina ya Lancruiser hardtop hospitalini hapo, Kaimu Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji wa Nzega Dkt. Anna Chaduo, aliishukuru serikali kwa kusema sasa hospitali yake itaweza kuwawahisha wagonjwa mahututi kutoka vituo vya afya kwenda hospitali ya Mji na hospitali nyingine za rufaa ndani na nje ya mkoa Tabora.
“Kila mwezi hospitali yetu inasafirisha wastani wa wagonjwa kumi na sita (16) wanaohitaji huduma za rufaa kwenda kwenye hospitali za rufaa ndani na nje ya Mkoa wa Tabora na hivyo, ujio wa gari hili utahakikisha wagonjwa wanawahishwa kupata matibabu hayo bila kuchelewa kama njia muhimu ya kuimarisha huduma za afya,” Alisema
Dkt. Chaduo anaeleza kuwa wagonjwa wenye mahitaji ya matibabu ya rufaa husafirishwa mara kwa mara kuelekea kwenye hospitali ya Kitete na Nkinga, zote ziko ndani ya Mkoa wa Tabora, na pia kwenda Hospitali nyingine za rufaa kama vile Bugando iliyoko jijini Mwanza na Hospitali ya Taifa – Muhimbili ya jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mganga Mkuu huyo alifafanua zaidi kuwa Hospitali yake hupokea na kuhudumia kati wagonjwa 550 hadi 700 kwa siku, ambao baadhi yao hupewa rufaa kutokea kwenye vituo vya afya viilivyoko mjini Nzega, ambao baadhi yao hulazimika kutumia gari la dharura kutokana na hali zao zinavyokuwa.
“Ujio wa gari hili utawezesha huduma za uzazi, wagonjwa ya nje (OPD) na wale wa dharura kupata huduma kwa haraka sana. Tunamshukuru sana Rais wa Tanzania kwa kuiona hospitali yetu na kutupatia gari hili,”
Akikabidhi gari hilo kwaniaba ya Mbunge wa Jimbo la Nzega Mjini Mhe. Hussein Bashe ambaye pia ni Waziri wa Kilimo, katibu wa Mbuge huyo Bw. Salim Abdulkadri aliwapongeza watumishi wa hopitali hiyo chini ya usimamizi dhabiti wa Mkurgenze mtendaji Bw. Shomary Mndolwa kuhakikisha wakazi wa jimbo hilo wanapata huduma nzuri za matibabu.
Bw. Abdulkadri aliitaka halmashauri ya mji wa Nzega kutumia gari hilo kuongeza chachu ya utendaji ili wananchi wawe na afya bora kwa zitakazowawezesha kufanya shughili mbalimbali za maendeleo.
NZEGA TOWN COUNCIL (HALMASHAURI YA MJI NZEGA)
Sanduku la Barua: S.L.P 256 NZEGA-TABORA
Simu ya Mezani: +255677003373
Simu ya Mkononi: +255677003373
Barua Pepe: td@nzegatc.go.tz
Haki miliki zote zimehifadhiwa na nzegatc 2017