WATUMISHI WA IDARA YA AFYA HALMASHAURI YA MJI WA NZEGA WAPATA MAFUNZO YA JINSI YA KUJILINDA WAKATI WAKUMUHUDUMIA MGONJWA WA MABARGI
Zaidi ya watumishi 50 kutoka vituo vya afya ,zahanati,Hospital wamepata Mafunzo ya jinsi yakujilinda wakati wakumuhudumia Mgonjwa wa Mabargi ,tukio hilo limefanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Nzega uliopo Ipazi
Mkufunzi wa mafunzo hayo kutoka Hospitali ya Mji wa Nzega Dkt.Tadeo Madikila amesema kuwa waameamua kutoa mafunzo hayo ikiwa niagizo la serikali na pia Mji wa Nzega upo njia panda unamwingiliano wa watu wengi kutoka mikoa mbali mbali na Nchi Jirani hivyo lazima tujiweke sawa ili hata kama Mgonjwa akitokea tujue namna ya kumhudumia huku na sisi tukijua namna ya kujikinga alisema
Akiwa ndani ya Mafunzo hayo akiyashuhudia namna yanavyoo endeshwa Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mji wa Nzega Dkt.Anna Chanduo amewataka wanamafunzo kuzingatia wanayo fundishwa kwakua wakienda kukosea wanaweza kupata madhara wao mwenyewe na wagonjwa wanao wahudumia .
Hivi karibuni kumekuwepo kwa kuzuka kwa Ugonjwa wa mlipuko wa Mabargi katika Nchi Jirani hivyo mafunzo haya yanaenda kuleta tija katika kupambana na Ugonjwa huo iwapo utatokea mafunzo yamefanyika kwa siku mbili kuanzia jana tarehe 10 Marchi mapaka leo tarehe 11 March ,2025 ambapo jana ilikuwa kwa nadharia na leo yanahitimishwa kwa vitendo .
NZEGA TOWN COUNCIL (HALMASHAURI YA MJI NZEGA)
Sanduku la Barua: S.L.P 256 NZEGA-TABORA
Simu ya Mezani: +255677003373
Simu ya Mkononi: +255677003373
Barua Pepe: td@nzegatc.go.tz
Haki miliki zote zimehifadhiwa na nzegatc 2017