Teknolojia ya Habari na Mawasiliano(TEHAMA) imeleta mapinduzi makubwa katika utendaji wa kazi katika taasisi mbalimba za Serikali.Halmashauiri ya Mji Nzega ni mojawapo ya taasisi ya Serikali ambayo imejikita katika matumizi ya TEHAMA.Kwa ujumla yamerahisisha na kuongeza kasi ya Utendaji kazi katika Halmashauri.
Mpaka sasa Halmashauri ina Mifumo zaidi ya kumi ambapo maandalizi ya kutumia mifumo mingine zaidi yanafanywa kwa kadiri ya mahitaji.
Mifumo hiyo ni kama ifuatavyo:
HCMIS – (LAWSON) Human Capital Management Information System –Mfumo wa kiutumishi.
LGRCIS (Local Government Revenue Collection Information System)- Mfumo wa Ukusanyaji wa Mapato katika Mamlaka za Serikali za Mitaa.Point Of Sale (POS) zimeunganishwa kwenye Mfumo huu .Hivyo makusanyo yoyote ya POS lazima yapitie kwenye mfumo wa huu.
EPICOR-Mfumo wa Malipo. Malipo yoyote katika Serikali za Mitaa lazima yapitie kwenye mfumo huu.
PREM (Primary Records Manager) -Mfumo wa Kutunza Taarifa za Wanafunzi wa Shule za Msingi .Uhamisho wa Wanafunzi hufanyika kwa kutumia mfumo huu.
BEMIS (Basic Education Management Information System) - Mfumo wa ukusanyaji wa Taarifa kwa Shule za Msingi na Sekondari.Soma zaidi http://www.equip-t.org/learning-innovations/emis/
GMS ( Government Mail System) - Mfumo wa Mawasiliano ya Barua Pepe Serikalini ambao unataka Taasisi zote za Serkaili kutumia barua pepe za Serikali zenye kikoi .go.tz
SIS (Schoo Information Syestem) -Mfumo wa ukusanyaji wa Taarifa za kila siku kwa Wanafunzi na Walimu juu ya ufundishaji kwa Shule za Msingi.Soma zaidi http://www.fhi360bi.org/user/tanzaniaSIS/#
PLAN REP (Planning, Budgeting And Reporting System) - Mfumo wa Mipango na Bajeti
FFARS (Facility Finacial Acounting and Reporting System) -Mfumo wa Kihasibu na Utoaji wa Taarifa za Fedha Kwenye Vituo vya Kutolea Huduma ikiwa ni kwenye Shule za Msingi, Sekondari, Vituo vya Afya pamoja na Zahanati.Mapokezi pamoja na matumizi lazima yapitie kwenye mfumo huu kwa vituo tajwa.
BARS (Biomtric Attendence Register System)-Mfumo wa Mahudhurio kwa watumishi
Tovuti ya Halmashauri www.nzegatc.go.tz
Matumizi ya Mifumo hii yamekuwa na mafanikio makubwa sio tu katika kuongeza kasi ya utendajikazi bali kwa sehemu kubwa imepunguza pia urasimu katika utoaji huduma kwa wananchi.
Tunawataka watumiaji wa mifumo kuzingatia Sheria ,Kanuni ,Taratibu na Miongozo mbalimbali ili kutunza usalama wa Taarifa mbalimbali za Serikali zilizoko katika Mifumo hii.
NZEGA TOWN COUNCIL (HALMASHAURI YA MJI NZEGA)
Sanduku la Barua: S.L.P 256 NZEGA-TABORA
Simu ya Mezani: +255677003373
Simu ya Mkononi: +255677003373
Barua Pepe: td@nzegatc.go.tz
Haki miliki zote zimehifadhiwa na nzegatc 2017