.
JENGO JIPYA LA MAKAO MAKUU YA HALMASHAURI YA MJI WA NZEGA LIMEKABIDHIWA
Katika kipindi cha miaka mitano ya Utawala wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Serikali ilikamilisha ujenzi wa jengo jipya la Utawala linalotumika kama Makao Makuu ya Halmashauri ya Mji Nzega.
Jengo hili lenye ghorofa moja, limegharimu zaidi ya shilingi bilioni tano za Kitanzania na limekabidhiwa rasmi Mwaka 2024. Kwa sasa linatumika kutoa huduma kwa Wananchi na liko eneo la Ipazi Kata ya Kitangili, Mjini Nzega.
Kazi zote za Ujenzi wa Jengo hili zimefanywa na Wakandarasi wa ndani ya nchi, huku Mkandarasi Mkuu akiwa ni Mzinga Holdings wa Mjini Morogoro. Mkandarasi huyu alitumia shilingi bilioni 4.8 kukamilisha awamu ya kwanza ya Ujenzi wa jengo hili lenye viwango sahihi kwa usalama wa Watushi na Wageni,
Pia nyingine ya mzawa, Nusaki Company Ltd, yenye makao yake makuu Mjini Nzega, ilitumia shilingi Milioni 870 kukamilisha shughuli za Umaliziaji wa jengo hili. Shughuli hizo ni Pamoja na ujenzi wa uzio kwa ajili ya usalama, pia kusimika taa za kuzunguka Jengo zima. Na barabara ya kuingia na kutoka.
Kampuni ya Nusaki Company Limited Imetumia kiasi hicho cha Fedha kujenga Barabara ya yenye urefu wa mita 240, inayounganisha jengo hili la makao makuu ya Halmashauri ya Mji Nzega na Barabara kuu ya Nzega Singida. Shughuli nyingine ni Pamoja na landscaping, na kuweka vitofali vidogo vidogo (paving blocks) ili kufanya mazingira ya jengo hili kuwa yenye mvuto na kutunza Mazingira.
Mbali ya ofisi za wataalamu mbali mbali, ndani ya jengo hili kuna kumbi mbili ndogo za mikutano, na ukumbi mkubwa wa kisasa wenye uwezo wa kukalisha watu 300 kwa wakati mmoja.
Jengo hili pia limewekewa mifumo yote muhimu ya TEHAMA ili kurahisisha mawasiliano, Tayari kampuni ya Mawasiliano nchini, TTCL imejenga mnara wa kurahisisha mawasiliano kwa Watumishi, Wananchi na wakazi wa eneo la IPAZI na maeneo Jirani
NZEGA TOWN COUNCIL (HALMASHAURI YA MJI NZEGA)
Sanduku la Barua: S.L.P 256 NZEGA-TABORA
Simu ya Mezani: +255677003373
Simu ya Mkononi: +255677003373
Barua Pepe: td@nzegatc.go.tz
Haki miliki zote zimehifadhiwa na nzegatc 2017