Katibu Tawala wa mkoa wa Tabora Ndugu Msalika R Makungu,amekemea vikali na kuwaonya wafanyakazi kwa kuwataka wasijihusishe na rushwa na kuongeza kuwa mkoa wa Tabora umejipambanua na hawatakuwa na msamaha kwa watumishi wala rushwa.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora akihutubia katika kikao cha tathmini ya utendaji kazi wa halmashauri ya mji wa Nzega
Akifungua kikao cha tathmini cha utendaji kazi katika halmashauri ya mji wa Nzega kilichofanyika tarehe 01/09/2020 katika ukumbi wa KKKT NZEGA, Katibu Tawala alitoa salaam kutoka kwa Mkuu wa Mkoa kwa washiriki akiipongeza Halmashauri ya Mji wa Nzega kwa kwenda mbali zaidi katika suala la kujitathmini ili kuboresha utendaji kazi katika Halmashauri. Aliwaomba wadau wote waliohudhuria kikao hicho kutoa maoni yao bila kumumunya maneno ili lengo halisi la Serikali ambalo linaitaka kila halmashauri kujitegemea kimapato liweze kufikiwa.
Aliipongeza Serikali kuu kwa kuzijengea uwezo halmashauri zote za serikali hali iliyopelekea kuondoa unyonge wa kuwa omba omba. Alionya kuwa suala la ukwepaji kodi unaofanywa na walipa kodi lazima huwa kuwa kuna ushirikiano na watendaji wa Serikali.
Katika kikao hicho Mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Nzega Ndugu Philemon Magesa aliwaomba washiriki kutoa tathmini ya utendaji kazi wa halmashauri ili kuboresha utendaji wa kazi.
Akitoa historia fupi ya halmashauri ya mji wa Nzega yenye vipao mbele vikuu vitatu ambavyo ni Mapato, Usafi wa mazingira na Utawala bora. Katika kutekeleza hayo Ndugu Magesa alibainisha kuwa halmashauri imefanikiwa kukusanya mapato kwa asilimia 88.41% hadi sasa na kuongeza kuwa halmashauri imekuwa ikipata hati safi tangu mwaka 2015.
Hata hivyo Mkurugenzi aliweza kubainisha changamoto ambazo zinapelekea kutofikia lengo halisi la ukusanyaji mapato ambazo ni mwitikio hafifu wa wananchi juu ya suala la ulipaji wa mapato, ongezeko la watu na baadhi ya wafanyabiashara kuchelewa kulipa kodi kwa wakati.
Katika kukabiliana na changamoto hizi Ndugu Magesa alibainisha kuwa halmashauri ina mikakati ya kupambana na changamoto hizo ikiwa ni pammoja na kuhamasisha wananchi kuchangia maendeleo, kujenga vizimba vya kukusanyia taka na kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa kulipa kodi.
Washiriki wa kikao hicho ambao walikuwa ni wadau kutoka kada mbalimbali walipata muda wa kuchangia ambapo kwa ujumla walitoa msisitizo kwa kuiomba halmashauri kuboresha huduma zake kwa wananchi.
NZEGA TOWN COUNCIL (HALMASHAURI YA MJI NZEGA)
Sanduku la Barua: S.L.P 256 NZEGA-TABORA
Simu ya Mezani: +255677003373
Simu ya Mkononi: +255677003373
Barua Pepe: td@nzegatc.go.tz
Haki miliki zote zimehifadhiwa na nzegatc 2017