Wakazi wa kata ya Mwanzoli na maeneo yanayo izunguka kata ya Mwanzoli wameondokana na adha waliyo kuwa wanaipata ya kutembea zaidi ya kilometa 20 kufata huduma ya Afya
hii nikutokana na kukamilika na kuanza kutumika kwa kituo cha Afya cha Kitengwe ambacho kimetumia kiasi cha Tsh.milioni 500 fedha kutoka serikali kuu.
kuanza kutumika kwa kituo hiki cha Afya kimeondoa shida walio kuwa wanaipata wakazi wa kata ya Mwanzoli ya kutembea umbali mrefu nakupelekea kutokea kwa vifo na hata wanawake kujifungulia njiani
Magreth Manumba mkazi wa Mwanzoli anasema hakuwahi kutegemea kujengewa kituo cha Afya ambacho kinafanya huduma ya upasuaji na mambo mengine ambayo yaliwafanya kutembea umbali mrefu wa kilometa 20 kufata hizo huduma kwenye Hospital ya Mji wa Nzega
kwa sasa anasema hata akipata shida ya kuumwa usiku anauwezo wa kutembea kwa miguu bila kuchoka anamshukuru sanaa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassani kwa kusikia kilio chao
kituo hiki cha Afya nimiongoni mwajitihada za serikali ya awamu ya sita kuhakikisha ina wapa tabasamu wananchi wak
NZEGA TOWN COUNCIL (HALMASHAURI YA MJI NZEGA)
Sanduku la Barua: S.L.P 256 NZEGA-TABORA
Simu ya Mezani: +255677003373
Simu ya Mkononi: +255677003373
Barua Pepe: td@nzegatc.go.tz
Haki miliki zote zimehifadhiwa na nzegatc 2017