Akiongea na Wajasiriamali waliohudhuria mafunzo ya Ujasriamali katika ukumbi wa Community Centre Kaimu Mkurugenzi Bwana Godson Harry aliwataka washiriki wa mafunzo hayo kuwa wasikivu na kuyashika mafundisho ili yalete mabadiliko katika maisha yao.
Alisema mafunzo hayo ni bure na yatafanyika kwa suki tatu (3) mfulilizo lengo likiwa ni kuwajengea uwezo wajasiria mali hao ili kuinuka kiuchumi.Aliwasisitiza wajasiriamali hao watumie fursa hiyo vizuri kujifunza na kutambua maswala mbalimbali ya kibishara kwani ni fursa pekee inayoweza kubadilisha maisha ya mtu endapo atazingatia atakachofundishwa.
Mafunzo hayo yanaendeshwa na Taasisi ya Mjasiriamali KWANZA ENTERPRISES chini ya Dr Didas Lunyungu.Mafunzo yanayofundishwa ni
Masomo ya Mapishi
Kazi za Mikono
Masomo ya ufugaji
Masomo ya bidhaa ya viwandani
Masomo ya kilimo
NZEGA TOWN COUNCIL (HALMASHAURI YA MJI NZEGA)
Sanduku la Barua: S.L.P 256 NZEGA-TABORA
Simu ya Mezani: +255677003373
Simu ya Mkononi: +255677003373
Barua Pepe: td@nzegatc.go.tz
Haki miliki zote zimehifadhiwa na nzegatc 2017