Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Nzega amewataka vijana kuwa na uzalendo, kucheza kwa kujituma na kwa moyo wote huku wakijua kuwa wanawakilisha Halmashauri ya Mji Nzega katika mashindano hayo.”Lengo la Halmashauri ni kuwaona mkifika katika ngazi ya Kiataifa na siyo kuishia katika ngazi ya Chini.” Alisema Mkurugenzi
Aliyaesma hayo leo alipokuwa anafungua mashindano ya michezo ya UMISETA kwa mwaka 2018 yanayofanyika katika viwanja vya polisi huku ikiwa imehdhuriwa na wanamichezo zaidi ya 360,Walimu wapatao 50 na mashabiki wasiopungua 600.
Aliongeza kuwa Halmashauri iko bega kwa bega nao kuhakikisha kuwa mashindano yatafanyika katika ngazi zote kama ilivyo lengo la Serikali licha ya changamoto za hapa na pale.Alisisitiza kuona changamoto kama ni sehemu ya fursa.
“Ndani ya miaka hii mitatu tumefanikiwa kwenda mbali sana,tumeshruki michezo mingi,tumeweza kupata tuzo mbalimbali,lakini kuna vijana wawili walishifika ngazi ya juu (nawapongeza sana) na mwaka huu nategemea mtaongezeka zaidi ya hao wawili”.Alisema Mkurugenzi
Aidha amewapongeza viongozi wote walioshiriki kuandaa mashindano hayo hadi kufikia hatua hiyo ambao ni Afisa Elimu Sekondari (Tabu Makanga), Meneja wa mashindano(Hamdani Shemzigwa), Mratibu wa mashindano(Singeli Mpemba) pamoja na Walimu wote kwa moyo uzalendo wa kujitolea.
Awali akimkaribisha mgeni rasmi Afisa Elimu Sekondari aliwaasa wanamichezo kuwa na nidhamu ya hali ya juu na kujituma ili waweze kufika mbali.
Mashindano hayo yanafanyika katika klasta 3 zilizogawanywa ili kurahisisha mchakato wa upatikanaji wa timu ya Halmashauri.
Michezo inayoshindanishwa ni pamoja na Mpira wa miguu wavulana na wasichana,mpira wa kikapu wavulana na wasichana,mpira wa wavu wavulana na wasichana,mpira wa mikono wavulana na wasichana,mpira wa pete kwa wasichana,mpira wa miguu maalum kwa wavulana,riadha maalum kwa wavulana na wasichana, riadha(mbio,mitupo na miruko), bao kwa wavulana na fani za ndani zikijumuisha kwaya,ngonjera,mashairi na ngoma za asili.
NZEGA TOWN COUNCIL (HALMASHAURI YA MJI NZEGA)
Sanduku la Barua: S.L.P 256 NZEGA-TABORA
Simu ya Mezani: +255677003373
Simu ya Mkononi: +255677003373
Barua Pepe: td@nzegatc.go.tz
Haki miliki zote zimehifadhiwa na nzegatc 2017