Makamu Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi Stephen Masato Wasira afurahishwa na Mji wa Nzega kwa kutekeleza Irani ya Chama cha mapinduzi kwa asilimia 100%
Akiwa kwenye ziara ya kikazi katika Halmashauri ya Mji wa Nzega aliyo ifanya siku ya jana March 15,2025 nakuwahutubia maelfu ya wanachama wa chama cha Mapinduzi na wananchi wa Mji wa Nzega kwenye ukumbi wa CCM uliopo eneo la Nzega Mjini
Makamu mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi alisema nimefurahishwa sana kuona ndani ya miaka mitano hii mmeweza kutekeleza Irani ya chama cha mapinduzi kwa asilimia100% hapa naona kila nikigusa sekta yoyote naona kabisa kuna jambo kubwa limefanyika mfano sekta ya Afya kuna zahanati 7 zimejengwa ,magari ya kubebea wagonjwa ya menunulia ,kwenye maji kila kaya ina maji mambo ni mengi nikianza kuyataja hapa siwezi kuya maliza alisema
Nae Juma Masanja Mkazi wa Nzega Mjini amekili kuwepo na mabadiliko makubwa ndani ya Mji wa Nzega akitolea Mfano wa swala la Maji miaka iliyo pita Mji wa Nzega tulipata sana tabu ya Maji watu tulishindwa kuoga kila siku lakini kwa sasa hakuna nyumba isiyo kuwa nabomba la maji linalo tiririsha maji mfululizo masaa 24,hivyo kwangu mimi naona huku Nzega Rais wetu hatu mdai kwakua kila sekta kagusa alisema
Makamu mwenyekiti alihitimisha ziara yake ndani ya Mji wa Nzega nakuelekea manispaa ya Tabora ambapo leo anaendelea na ziara katika wilaya ya Sikonge
NZEGA TOWN COUNCIL (HALMASHAURI YA MJI NZEGA)
Sanduku la Barua: S.L.P 256 NZEGA-TABORA
Simu ya Mezani: +255677003373
Simu ya Mkononi: +255677003373
Barua Pepe: td@nzegatc.go.tz
Haki miliki zote zimehifadhiwa na nzegatc 2017