HALMASHAURI YA MJI WA NZEGA YAPATA HATI SAFI
Mkutano maalumu wa Baraza la Madiwani kujadili taarifa ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali kwa mwaka wa fedha 2023/2024
umefanyika jana tarehe 17 june ,2025 kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Nzega uliopo eneo la ipazi ambapo kaimu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Ndg.Hamza Zonga alisoma ripoti ya Ukaguzi na udhibiti wa hesabu za serikali
Taarifa inaonyesha Halmashauri ya Mji wa Nzega imepata Hati inayoridhisha au kwajina jingine Hati Safi
Hati hii hutolewa pale Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) anaporidhika kuwa taarifa za fedha alizokagua zimeandaliwa kwa usahihi na kwa kuzingatia viwango vya uhasibu vya kimataifa vya uandaaji wa Taarifa za fedha (IPSAS).
Mhe.Sauda S.Mtondoo Mkuu wa Wilaya ya Igunga akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe.Paul Chacha kwenye baraza hilo maalumu ametoa hongera kwa Halmashauri ya Mji wa Nzega kwa kupata Hati hiyo safi na kwamba wakuu wa idara na vitengo waendelee kufanya kazi kwakufata miongozo inavyo takiwa
aidha akatumia furusa hiyo kuwa shukuru waheshiwa madiwani wa Mji wa Nzega kwakujitoa kwao katika kipindi hiki cha miaka mitano kwani wameufanya Mji wa Nzega uendelee kung'aa
NZEGA TOWN COUNCIL (HALMASHAURI YA MJI NZEGA)
Sanduku la Barua: S.L.P 256 NZEGA-TABORA
Simu ya Mezani: +255677003373
Simu ya Mkononi: +255677003373
Barua Pepe: td@nzegatc.go.tz
Haki miliki zote zimehifadhiwa na nzegatc 2017