Kaimu Mkurugenzi Ndg. David Rikanga akifungua mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Community Cetre
Kabla ya kufungua Mkutano huo alikaribishwa na Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Bwana Godson Harry.Akimkaribisha Kaimu Mkurugenzi Bwana Harry alisema kuwa lengo kubwa la Mkutano huo ni kutambilisha rasmi SACCOS ya Wanawake ambayo msingi wake mkubwa ni uzinduzi wa Jukwaa la Kiuchumi la Wanawake Halmashauri ya Mji Nzega.Alisema kwamba wakati wa uzinduzi wa jukwaa hilo walikubaliana kuunda chombo ambacho ni SACCOS.
NZEGA TC Wanawake SACCOS ilianza rasmi baada kufanya Mkutano wake Mkuu wa Kwanza wa uanzilishi tarehe 15/09/2017.Mkutano huo ulihudhuriwa na wanachama waanzilishi takriban 120.
Alitaja pia shughuli zitakazofanyika katika mkutano huo kuwa ni pamoja na Taarifa fupi ya Utambulisho rasmi wa SACCOS ya wanawake,Masuala ya Jukwaa la Wanawake,Maelezo ya Jukwaa la Wanawake Kimkoa,Maandalizi ya siku ya Wanawake Duniani,Uchaguzi wa katibu wa Jukwaa la Wanawake pamoja na viongozi wa SACCOS.
Akifungua Mkutano huo Kaimu Mkurugenzi aliwapongeza wanawake hao kwa harakati zao za maendeleo na kwamba SACCOS hiyo itaongeza mzunguko wa hela katika Halmashauri.Aliwapongeza pia kwa kujitokeza kwa wingi kuchukua mikopo.
Alisisitiza kuwa Halmashauri itaendelea kutenga asilimia 10% kwaajili ya Wanawake na Vijana.
Ametoa wito kwa vijana kujitikeza kwa wingi kuchukua mikopo kwani wamekuwa wakilegalega.
Katika Mkutano huo Zuhura Salum alichaguliwa kuwa katibu wa Jukwaa la Wanawake.
VIONGOZI WA SACCOS.
-HALIMA
-HAPPINESS
NZEGA TOWN COUNCIL (HALMASHAURI YA MJI NZEGA)
Sanduku la Barua: S.L.P 256 NZEGA-TABORA
Simu ya Mezani: +255677003373
Simu ya Mkononi: +255677003373
Barua Pepe: td@nzegatc.go.tz
Haki miliki zote zimehifadhiwa na nzegatc 2017