Mkuu wa Mkoa wa Tabora Ndg.Aggrey Mwanri amezindua upandaji wa miti kwa vyuo katika Halmashauri ya Mji Nzega.Akiongea na Wanafunzi wa Chuo cha FDC Kitongo pamoja watumishi wa Halmashauri Mkuu wa Mkoa alisisitiza kuwa anataka Mkoa wa Tabora uwe Mwanga bora unaoangaza katika upandaji wa miti na utunzaji wa mazingira.Alimsifu Mkurugenzi pamoja na Mkuu wa Wilaya kwa kasi kubwa wanayoendanayo katika upandaji wa miti. Hadi sasa Halmashauri imeweza kupanda jumla ya miti 36,109 katika maeneo mbalimbali ikiwemo kando kando ya Barabara za Tabora, Shinyanga na Singida, Shule za Msingi na Sekondari, Mitaa ya Mjini, Watu binafsi pamoja na Taasisi za Serikali na Mashirika kama vile
Akiwa na Wanachuo hao jumla ya miti 100 ilipandwa na wanachuo wameahidi kuitunza na kwamba itakuwa ni kumbukumbu nzuri kwao pindi watakapohitimu chuo.
Mkuu wa Mkoa aliwataka kuhakikisha kuwa miti hiyo haifi na kwa vile wameahidi wenyewe basi ni jambo jema na kwamba mda wowote atakuwa anatembelea kuona maendeleo yake.
NZEGA TOWN COUNCIL (HALMASHAURI YA MJI NZEGA)
Sanduku la Barua: S.L.P 256 NZEGA-TABORA
Simu ya Mezani: +255677003373
Simu ya Mkononi: +255677003373
Barua Pepe: td@nzegatc.go.tz
Haki miliki zote zimehifadhiwa na nzegatc 2017