Mwenge wa Uhuru umezindua Miradi ya maendeleo yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni mbili na milioni miatano Kwenye Halmashauri ya Mji wa Nzega iliyoko Mkoa wa Tabora.
Mbio za Mwenge huo asubuhi ya Tarehe 20/09/2023, zilianza kwa makabidhiano ya Mwenge huo kutoka kwa Halmashauri ya Wilaya ya Nzega, ambapo Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Naitapwaki Tukai aliwakaribisha rasimi wakimbiza Mwenge na Kusema Wilaya yake iko tayari kwa ukaguzi wa shughuli na Miradi ya maendeleo na kuzindua miradi hiyo.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji – Nzega, Bwana Shomary Mndolwa, alisema miradi ilyozinduliwa ni pamoja na kuweka jiwe la msingi ujenzi wa mradi wa mabwawa ya kutibu maji taka uliojengwa kwa gharama ya Shs Bilioni 1 na milioni miatano.
Pia Mwenge wa Uhuru uliweka jiwe la Msingi kwenye mradi wa maduka mjini Nzega na pia Kuzindua vyumba viwili vya madarasa na vyoo katika Shule ya Msingi ya Nyasa II. Ukiwa katika eneo la Uwanja wa Ndege, Mwenge wa Uhuru ulikagua shughuli za vijana wajasiriamali na kushiriki shughuli za upandaji miti.
Pia Mwenge wa Uhuru uliweka jiwe la msingi katika jengo jipya la wodi ya Baba, Mama na Mtoto Zahanati ya kata Miguwa. Baadaye msafara huo ulikagua na kuona shughuli za Uhamasishaji wa Lishe na kuona shughuli za vikundi vya wajasiriamali vya Mjini Nzega.
Katika kutimiza kauli mbia ya mwaka huu, msafara wa Mwenge wa Uhuru ulishiriki pia shughuli za Upandaji Miti ili kutunza mazingira.
NZEGA TOWN COUNCIL (HALMASHAURI YA MJI NZEGA)
Sanduku la Barua: S.L.P 256 NZEGA-TABORA
Simu ya Mezani: +255677003373
Simu ya Mkononi: +255677003373
Barua Pepe: td@nzegatc.go.tz
Haki miliki zote zimehifadhiwa na nzegatc 2017