MWENYEKITI wa umoja wa vijana taifa Kheri James amempongeza Mkuu wa Wilaya ya Nzega Godfrey Ngupula kwa usimamiza wa maendeleo ya Wilaya kwa uadilifu wa hali ya juu.
Pongezi hizo alizitoa wakati alipotembelea wilayani hapa, tarehe 1 Oktoba 2018 kuangalia uhai wa Jumuia ya Vijana ikiwa ni pamoja na namana gani wanavyowezeshwa kuipitia asilimia kumi ya mapato ya ndani ya halmashauri.
Alisema nimeridhika kwa namna Mkuu wa wilaya ya Nzega anavyojituma katika kasimamia miradi ya maendeleo bila kupapasa macho na kwa haki.
Aidha alisema nimefurahishwa na jinsi alivyotekeleza agizo la Waziri mkuu Kasim Majaliwa katika kushughulikia migogoro ya ardhi iliyokuwa imedumu kwa mda mrefu bila ufumbuzi.
“Unajua lazima penye ukweli tuzungumze ukweli hapa nzega mmepata Mkuu wa Wilaya anayejiamini anayesimamia maagizo ya Serikli na kujali maslahi ya umma”. Alisema James
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Nzega Godfrey Ngupula alisema halmashauri zote katika wilaya ya Nzega zinatekeleza agizo la Serikali la kuwewezesha kiuchumi wakinamama,vijana na walemavu kuipitia asilimia kumi ya mapato ya ndani.
Ngupula alisema licha ya changamoto nyingi katika kutoa mikopo hiyo kwa vikundi vya akina mama na vijana lakini hali ni nzuri na vikundi vinaendelea kujisajili ili viweze kupatiwa mikopo.
Naye mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Nzega Amos Kanuda alisema Chama kitaendelea kusisitiza Serikali juu ya uwezeshaji wa kina mama,vijana na walemavu kama ilani ya uchaguzi inavyo elekeza.
Alisema tumekuwa na ushirikiano mzuri kati yetu na jumuiya ya Vijana, Serikali pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo ili kuhakikisha tunajenga Nzega ya kimkakati na yenye maendeleo ya haraka.
NZEGA TOWN COUNCIL (HALMASHAURI YA MJI NZEGA)
Sanduku la Barua: S.L.P 256 NZEGA-TABORA
Simu ya Mezani: +255677003373
Simu ya Mkononi: +255677003373
Barua Pepe: td@nzegatc.go.tz
Haki miliki zote zimehifadhiwa na nzegatc 2017