Na James Kamala
Watumishi wa Umma katika Halmashauri ya Mji wa Nzega wamepatiwa mafunzo ya namna bora ya kutumia mifumo ya kielekktroniki ili kuimarisha utendaji kazi katika utumishi wa umma.
Mafunzo hayo yaliwezeshwa na kuendeshwa na maafisa kutoka Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, yanalenga kuwawezesha watumishi wa serikali kutumia mfumo huo kwa wepesi na uharaka zaidi katika utendaji kazi wa kila siku.
Mifumo iliyofundishwa ni pamoja na Mfumo wa Kielektroni wa Uhamisho (ESS) (ess.utumishi.go.tz) ambapo mtumishi akishajisajiri ataweza kutumia wa mtumishi na taasisi katika utumishi wa umma (PEPMIS na PIPMIS)
Lengo la mafunzo hayo ya siku moja kuwajengea watumishi hao wa umma uelewa wepesi ili waweze kuhama salama kutoka kwenye mifumo ya zamani kama vile ule wa kupima utendaji kazi -OPRAS, na mingineyo iliyokuwa haifanyiki kwa njia ya mtandao
“Mifumo ya PEPMIS na PIPMIS itakuwa na taarifa zote za mwajirwa pamoja na majukumu ya kazi, pia Mtumishi ataweza kupata hudama nyngine kwa njia ya kielektoniki kama vile kupima utendaji kazi na kuomba uhamisho kutoka eneo moja la kazi kwenda lingie au taasisi moja kwenda Nyingine,” Alisema Bi. Elizabeth Makyao, Mkurugenzi Msaidizi kutoka Ofisi ya Rais - Utumishi
Bi. Makyao aliwaondoa hofu watumishi wa Halmashauri ya Mji wa Nzega kuwa matumizi ya mifumo hiyo ni rafiki sana na hivyo kila mtumishi anaweza kuitumia bila usumbufu wowote. Ameongeza kuwa mifumo hiyo inatumia vifurushi vya kawaida vya data, na hivyo gaharama yake ni rafiki kwa watumishi wa Umma.
Naye mwezeshaji wa mafunzo hayo Bwana Aidan Lukasi kutoka Ofisi ya Rais – Utumishi, alsema mifumo hiyo itarahisiha upimaji wa utendaji Kazi wa kila Mtumishi wa Umma. Aliongeza kuwa mifumo hiyo itawaondolea usumbufu waliokuwa wakikabiliana nao watumishi wa umma kwa kutumia mifumo ya zamani.
Usumbufu huo, alisema Bwana Lukasi kuwa pamoja na kupotea kwa nyaraka au kucheleweshewa vitu mbali mbali watumishi wa umaa na hivyo kulazimia kurudia rudia kufanya kazi mbali mbali bila sababu za msingi
NZEGA TOWN COUNCIL (HALMASHAURI YA MJI NZEGA)
Sanduku la Barua: S.L.P 256 NZEGA-TABORA
Simu ya Mezani: +255677003373
Simu ya Mkononi: +255677003373
Barua Pepe: td@nzegatc.go.tz
Haki miliki zote zimehifadhiwa na nzegatc 2017