Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Suleman Jaffo amesema serikali ipo tayari kujenga daraja la mto Nhobola lilipo katika kata ya Mbogwe Halmashauri ya Mji wa Nzega ili kuondoa adha inayowakabili wananchi wa kata hiyo wakati wa kuvuka hasa nyakati za mvua kutokana mafuriko.
Jaffo ametoa kauli hiyo leo wakati akiongea na wananchi wa kata hiyo akiwa katika ziara ya kikazi katika Halmashauri ya Mji Nzega ambapo ametembelea eneo litakolojengwa daraja hilo ili kujiridhisha na tadhimini aliyokabidhiwa na wataalamu juu ya ujenzi wa daraja hilo.
"Lengo kubwa la mimi kufika katika eneo hili ni kuona na kijiridhisha juu ya eneo litakapojengwa daraja ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi ya Rais John Magufuli wakati wa kampeni za uchaguzi Mkuu mwaka 2015 kwasababu mvua zikinyesha hapa watu wanashindwa kuvuka kutokana na mto kufurika na mbunge wenu amekuwa akinieleza kuhusu daraja hili na ndio maana leo nimeamua kuja kuona daraja lenyeweā€¯.Alisema Jaffo.
Alieleza kuwa Wizara yake imetenga jumla Tshs bilioni 273 kwaajili ya ujenzi wa miundombinu ya barabara na katika fedha hizo ujenzi wa daraja la Nhobola lipo
ambapo amewataka wananchi wa Tabora kuacha tabia ya kuhujumu miundombinu ya barabara hasa madaraja kwa kufungua vyuma.
"Mkoa wa Tabora umekuwa na matukio mengi ya kuhujumu miundombinu hasa kufungua vyuma kwenye kingo za barabara na madaraja. Niwatake wananchi wa eneo hili kuwa walinzi katika kulinda miundombinu ya daraja pindi litakapojengwa kwani pamoja na kuomba kuwekewa taa haitakuwa mwarobaini wa wizi kama wenyewe hamtakuwa wailinzi" Alisisitiza waziri huyo.
Awali akiwa katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya Nzeg Mh; Jaffo alimkaribisha Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora ambaye aliteuliwa na Mhe.Rais hivi karibuni pia amewataka Wakurugenzi kuhakikisha kwamba hoja zote zilizoibuliwa na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali zinapatiwa majibu kwa wakati.
NZEGA TOWN COUNCIL (HALMASHAURI YA MJI NZEGA)
Sanduku la Barua: S.L.P 256 NZEGA-TABORA
Simu ya Mezani: +255677003373
Simu ya Mkononi: +255677003373
Barua Pepe: td@nzegatc.go.tz
Haki miliki zote zimehifadhiwa na nzegatc 2017