Mkuu wa Mkoa wa Tabora Ndg.Aggrey Mwanri amewata wadau wa elimu wanaosimamia sekta ya Elimu kuhakikisha wanasimamia kauli mbiu ya Mkoa wa Tabora inayosema “Tabora bila sifuri,utoro, utumikishaji watoto mashambani, na mimba za utotoni inawezekana kila mmoja atomize wajibu wake .
Mwanri aliyasema hayo alipokuwa anazungumza na Walimu Wakuu wa Shule za Sekondari na Msingi,Maafisa elimu Kata pamoja na Maafisa Elimu wa Halmashauri za Nzega Mji na Nzega Vijijini katika kikao kazi kilichofanyika katika ukumbi wa FDC Kitongo hivi karibuni.Lengo la kikao kazi hhicho ni kukumbushana mambo mbalimbali yanayohusiana na Elimu.
Mkuu wa Mkoa aliambatana na Katibu Tawala Mkoa Bwana Msalika Makungu.
Mkuu wa Mkoa akiongea na Wataalam hao alisisitiza mambo mbalimbali ya Kielimu huku akianza kwa kulezea historia ya Mkoa wa Tabora kuwa ni chimbuko la wasomi na viongozi mbalimbali akiwepo Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere
Alisisitiza swala la utoro mashuleni huku akiwataka Maafisa Elimu Kata kuhakikisha wanawachukulia hatua wanafunzi watoro pamoja na Wazazi wao.Alisema kuwa takwimu za hivi karibuni zinaonyesa kuwa watoto 6,206 kati ya 11,004 ambao walikuwa watoro ndio wamerudi darasani kwa ajili ya kuendelea na masomo kama alivyokuwa ameagiza.
Alisema hakuna sababu ya kufanya mzazi ashindwe kumpeleka shule mtoto wake kwani Serikali ya Awamu ya Tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeondoa vikwazo vyote vilivyokuwa vikisababisha ugumu kwa mzazi. Watoto waliorudi ni zaidi ya asilimia 50 na waliobaki wanaofikia 4,998 na kutaka waanze mara moja kutafutwa walipo kwa ajili ya kurudishwa madarasani
Awali Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu amewataka kubaki shuleni kufundisha na kuacha tabia ya kutokuwepo katika maeneo yao ya kazi.Walimu wamekuwa wakitumia mda mwingi kwenda kufuatilia mambo yao Halmashauri na kuacha majukumu yao ya msingi.Amewataka Maafisa Elimu pamoja na Maafisa Utumishi kuhakikisha wanatatua matatizo ya Walimu ili waendelee kubaki katika maeneo yao ya kazi kipindi chote.
NZEGA TOWN COUNCIL (HALMASHAURI YA MJI NZEGA)
Sanduku la Barua: S.L.P 256 NZEGA-TABORA
Simu ya Mezani: +255677003373
Simu ya Mkononi: +255677003373
Barua Pepe: td@nzegatc.go.tz
Haki miliki zote zimehifadhiwa na nzegatc 2017