TIMU YA UONGOZI YA HALMASHAURI YA MJI WA NZEGA YA FANYA ZIARA YA UKAGUZI WA MIRADI YENYE THAMANI YA TSH.BILIONI 1.8
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Nzega Bi.Joyce Emanuel ameiogoza timu ya uongozi ya Halmashauri ya Mji wa Nzega katika ukaguzi wa Miradi mitatu yenye thamani ya Tsh.Bilioni 1.8
Zoezi hili limefanyika siku ya leo Alhamisi ikiwa ni utaratibu wa kila mwezi kwa timu hii kufanya ukaguzi wa miradi mbali mbali inayo tekelezwa ndani ya Halmashauri
Miradi hiyo ni jengo lenye madarasa matatu na ofisi moja ,matundu sita ya vyoo vya wasichana katika shule ya Msingi Tazengwa yenye thamani ya Tsh.milioni 92.2 ambazo ni fedha kutoka BOOST
Pia katika shule ya msingi Ipilili mradi ulio kaguliwa ni jengo la madarasa matatu na ofisi moja ,matundu sita ya vyoo vya wasichana vyote ikiwa na thamani ya Tsh.milioni 92.2 fedha hizi zikiwa zimetoka BOOST
Pamoja nahayo pia katika Kijiji cha makomelo mradi wa ujenzi wa shule ya sekondari ya amali (ufundi) imekaguliwa na timu ya uongozi ambapo jumla ya majengo 15 yanajengwa ambayo yanajumuisha madarasa ,mabweni ya wavulana na wasichana ,maabara ya fizikia,bailojia na kemia,jengo la TEHAMA,karakana za ufundi , vyoo vya wa sichana na wa vulana thamani ya mradi huu ni Tsh.bilioni 1.6 fedha hizi zimetoka SEQIUP
Miradi ya shule ya msingi ipilili na Tazengwa imefikia asilimia 98% huku mradi wa shule ya sekondari ya Amali ukiwa unaendelea na pia umefikia asilimia 58 miradi hii ya Shule ya Msingi Ipilili na Shule ya Msingi Tazegwa inaenda kuongeza mazingira mazuri ya ufundishaji na ujifunzaji
Huku shule ya sekondari katika Kijiji cha Makomelo itakuwa shule ya kwanza ya Amali (Ufundi) katika wilaya ya nzega ambapo inatarajiwa kuleta ajira za kujiali nyingi zaidi baada ya kukamilika ,hii imekuwa nimiongoni mwa jitihada zinazo fanywa na serikali ya Awamu ya sita ikiongozwa na Dk.Samia Suluhu Hassani Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
NZEGA TOWN COUNCIL (HALMASHAURI YA MJI NZEGA)
Sanduku la Barua: S.L.P 256 NZEGA-TABORA
Simu ya Mezani: +255677003373
Simu ya Mkononi: +255677003373
Barua Pepe: td@nzegatc.go.tz
Haki miliki zote zimehifadhiwa na nzegatc 2017