ZIARA YA TIMU YA UKAGUZI YA MIRADI YA HALMASHAURI
Kamati ya ukaguzi ya miradi ya halmashauri leo tarehe 20/10/2022 imetembelea miradi inayoendelea kujengwa katika Halmashauri.Miradi iliyotembelewa ni ujenzi wa sekondari mpya (SEQUIP) katika mtaa wa uwanja wa ndege kata ya Nzega Mjini Mashariki na ujenzi wa Kituo cha Afya Kitengwe.
Ikiwa katika mtaa wa Uwanja wa ndege kukagua ujenzi wa shule ya Sekondari kamati hiyo ikiongozwa na Kaimu Mkurugenzi Bi.LEAH KIBAKI ilifanya ukaguzi wa majengo yafuatayo
Kamati iliridhika na hatua iliyofikiwa na ujenzi huo pamoja na ubora wake japo kuna marekebisho madogo ambayo kamati ilimwaagiza fundi kukamilisha.viongozi paomja na wajumbe wa mtaa huo waliokuwepo kwenye ukaguzi huo waliishauri kamati kuweka barabara katika eneo hilo ili kuondoa wasiwasi kwa wananchi waliojenga jirani na eneo la shule.Kaimu Mkurugenzi akijibu hoja hiyo aliwaakikishia kuwa swala hilo litafanyiwa kazi mapema iwezekanavyo.aliwashukuru pia wajumbe hao kwa ushirikiano wao katiak utekelezaji wa mradi.
Ikiwa katika kata ya Mwanzoli kamati imekagua ujenzi wa Kituo cha Afya Kitengwe ambapo majengo yafuatayo yamekaguliwa:
Kamati imeridhika na hatua ya ujenzi iliyofikiwa
NZEGA TOWN COUNCIL (HALMASHAURI YA MJI NZEGA)
Sanduku la Barua: S.L.P 256 NZEGA-TABORA
Simu ya Mezani: +255677003373
Simu ya Mkononi: +255677003373
Barua Pepe: td@nzegatc.go.tz
Haki miliki zote zimehifadhiwa na nzegatc 2017