Mkuu wa Wilaya Nzega Mhe.Godfrey Ngupula amesema Serikali ya awamu ya tano inathamini afya za wananchi dio maana imeendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuboresha afya kwa upande wa kinga na tiba.
Ngupula amesema hay oleo wakati akizindua utoaji wa chanjo ya kuzuia saratani ya mlango wa kizazi kwa wasichana wenye umri wa miaka 14 iliyofanyika katika Zahanati ya Samora ambapo alieleza kuwa katika kuelekea Tanzania ya viwanda na uchumi wakati, Serikali kupitia Wizara ya Afya inahakikisha hakuna mwananchi atakayeshindwa kufanya kazi kwa kusumbuliwa na maradhi.
“Mwaka huu wa 2018,Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeamua kuanzisha chanjoya kukinga saratani ya mlango wa kizazi ili kuwakinga mabinti dhidi ya saratani ya mlango wa kizazi.” Alisema Ngupula.
Aliongeza kuwa kuwa takwimu zinaonyesha takriban wagonjwa wapya elfu hamsini kila mwaka hugundulika kuwa na saratani za aina mbalmbali hapa nchini na wagonjwa elfu kumi na tatu kati ya hao sawa na 26% ndio wanaofanikiwa kupata matibabu.
Alifafanua kuwa, Takwimu kutoka Taasisis ya Saratani ya Ocean Road za mwaka 2016/2017 zinaonesha kwamba saratani ya mlango wa kizazi inaongoza kwa kuwa na wagonjwa wengi kwa 32.8% na saratani ya mlango wa kizazi huchangia asilimia 38 ya vifo vitokanavyo na saratani.
Alisema ametaarifiwa kuwa, chanjo hiyo ni salama na imethibitishwa na shirika la Afya Duniani (WHO) na inatumika katika nchi nyingi duniani na imeonyesha uwezo mkubwa sana wa kuzuia saratani ya mlango wa kizazi.Hivyo anatumaini kuwa uanzishwaji wa chanjo hiyo utaendeleza mapambano dhidi ya saratani
Alieleza kuwa Mkoa wetu wa Tabora unatarajia kuchanja jumla ya wasichana 32,164 na katika Halmashauri yetu ya Mji tunatarajia kuchanja jumla ya wasichana 1,946 kwa mwaka huu wa 2018.
Aidha alisisitiza kuwa Serikali inatoa chanjo hii ya saratani ya mlango wa kizazi bila malipo yoyote katika vituo vinavyotoa huduma za chanjo vya Serikali, Mashirika ya Dini na vya Taasisi binafsi.
Mkuu wa Wilaya ametoa wito kwa wanawake wote wajitokeze kwa wingi katika hospitali mbalimbali nchini illi waweze kufaniwa uchunguzi dhidi ya ugonjwa wa saratani kila wakati kunapopatikana fursa hiyo. “Ninawataka Waganga Wakuu wa Wilaya kuandaa kambi za wazazi angalau mara tatu kwa mwaka ili kutoa fursa kwa wanawake wengi zaidi kupima saratani ya matiti nay a mlango wa kizazi.” Alisema Mkuu wa Wilaya.
Aliipongeza Wizara ya Afya kwa kushirikiana vyema na wadau mbalimbali wa maendeleo ndani na nje ya nchi, na kufanya jitihada zinazoonekana za kuboresha utoaji wa chanjo ya kuzuia saratani ya mlango wa kizazi kwa lengo la kupunguza vifo vitokanavyo na ugonjwa huo.
Pia aliwashukuru wadau mbalimbali waliochangia katika kufanikisha utoaji wa huduma za chanjo hapa nchini akiwemo shirika la Global Vaccine Alliance (DAVI), Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO), Shirika la kuhudumia Watoto (UNICEF), Clinton Health Access Initiative (CHAI), John Snow Inc (JSI) pamoja na wadau wengine kwa misaada yao.
NZEGA TOWN COUNCIL (HALMASHAURI YA MJI NZEGA)
Sanduku la Barua: S.L.P 256 NZEGA-TABORA
Simu ya Mezani: +255677003373
Simu ya Mkononi: +255677003373
Barua Pepe: td@nzegatc.go.tz
Haki miliki zote zimehifadhiwa na nzegatc 2017