Mkuu wa Wilaya ya Nzega ACP.ADVERA BULIMBA, tarehe 28.09.2022 katika ukumbi wa SERENE ulioko katika Halmashauri ya mji Nzega amezindua Mwongozo wa elimu kwa shule za Msingi na Sekondari.Miongozo hiyo iko mitatu na imezndiliwa kitaifa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.wadau mbalimbali waliohudhuria kikao ni pamoja na madiwani,maafisa kata,vijiji na mitaa,maafisa Elimu Kata,Wakuu wa Idara na Vitengo,wadhibiti obora elimu,Afisa Tarafa,wakuu wa shule za msingi na sekondari pamoja na wazee maarufu.
Akiongea na wadau hao wa elimu Mkuu wa Wilaya,alisema kuwa ukiona mkakati wa elimu unazindiliwa ujue kuna changamoto zinazojitokeza na kwamba kila mmoja atapimwa kulingana na utekelezaji wa miongozo hiyo.
Amewataka wadau hao kuhakikisha kuwa swala la kushuka kwa elimu halitatokea tena katika Wilaya yake.
Amewataka maafisa elimu kata kuwajibika na kama hawawezi ahame mwenyewe kabla ya yeye kuchuka hatua.Amewata pia kuhakikisha wanaiarisha ufuatiliaji wa elimu hasa utoro mashuleni.
Amesisitiza nidhamu ikawe msingi wa kazi
Ametaka elimu ikawe ajenda ya kudumu katika vikoa katika ngazi zote za Wilaya.
“Simamieni miongozo ya uteuzi kwa haki (nyie maafisa elimu) kama mtu hana sifa msimteue” Alisema Mkuu wa Wilaya.
Amewasititiza wazazi wanaokwamisha mikakati ye elimu wachukuliwe hatua.amesema hayo kupitia kwa wazee maarufu waiohudhuria kikao hicho akiwemo Marry Igogo.
Ameiopongeza Halmashauri ya mji Nzega kwa ufaulu wa jumla kuanzia darasa la nne,la saba,form two, form iv na form six kwa ufaulu wa asilimia mia moja.
Mkuu wa Wilaya ameahidi kutolala hadi hali ya elimu iimarike.
Amehoji pia kama fedha zinazotolewa na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mh.Samia Hassan Suluhu zina tatua changamoto za kielimu hasa miundombinu ya shule ,madawati na chakula.
Amewataka viongozi wa kuhakikisha wanatatua kero za walimu hasa stahiki zao zilipwe kwa wakati ili kuwaondolea usumbufu.
“Kila mwanafunzi mwenye umri wa kwenda shule aandikishwe na kuhakikisha wanakwenda shule.Kazi hii wasimamie watendaji wakishirikiana Maafisa Elimu Kata” Alisema Mkuu wa Wilaya.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Nzega Ndugu. Shomary S. Mndolwa katika kikao hicho cha ufunguzi wa Miongozo ya Elimu kwa shule za msingi na secondary alisema kuwa Halmshauri imepokea fedha kutoka kwaajili ya uimarishaji wa elimu hasa katika eneo la miundo mbinu. “Halmshauri imetenga pia fedha kiasi cha millioni 480 kutoka mapato ya ndani kwaajili ya uboreshaji wa miundombinu ya Elimu”.Alisema Mkurugenzi
Amesema kuwa ili kuinua kiwango cha ufaulu katika Halmashauri atatoa motisha kwa shule zitakazo fanya vizuri.”Nataka kuahidi, shule itakayoongoza kwa ufaulu itapewa shilingi milioni moja (1,000,000) na Mwalimu Mkuu atapewa shilingi laki tano (500,000)”Alisema Mkurugenzi
AFISA ELIMU SEKONDARI BI.LULU B NCHIHA Akisoma taarifa yake mbele ya mgeni Rasmi alisema kuwa Ofisi ya Rais TAMISEMI imekuwa ikifanya ufuatiliaji na tathmini ya mara kwa mara ili kuona maendeleo ya Elimu ya Msingi na Sekondari. Tathmini ya hivi karibuni imebaini uwepo wa mafanikio na changamoto kadhaa ambazo kwa pamoja zimesababishwa na uwekezaji mkubwa unaofanywa na Serikali katika Sekta hii. Ili kukabiliana na changamoto zinazoikabili Sekta hii na hivyo kuboresha Elimu ya Msingi na Sekondari Nchini, Serikali imeandaa miongozo mitatu za kuzingatiwa katika usimamizi na uendeshaji wa shule:-
LENGO LA MWONGOZO NA MKAKATI WA KUIMARISHA UFUNDISHAJI KATIKA NGAZI YA ELIMU MSINGI NA SEKONDARI
AFIS ELIMU MSINGI NDG.AJALII M MARUMWENGU alitoa ufafanuzi juu ya miongozo hiyo kuwa ni maagizo ya Serikali na lazima yatekelezwe kwa ufanisi.Alisema kuwa miongozi hiyo ilizinduliwa Kimkoa tarehe 16/08/2022 wakati wa umitashumta.
WADAU WA ELIMU
Mzee maarufu, MZEE SAMOTA alisema kuwa atachangia baiskeli mia moja(100) kwa shule ambayo itaingia kumi bora katika Mkoa wa Tabora..hii ni katika harakati za kuinua kiwango cha Elimu katika Wilaya ya Nzega
Naye Mzee maarufu Mama Merry Igogo wakati akichangia alimwomba Mzee Samota kuwa mfadhili wa Walimu Wakuu.Alimwomba awafadhili Mabati ili waweze kujenga na kuishi katika mazingira mazuri ambayo yatawawezesha kufanya kazi vizuri.
Madiwani pamoja na wajumbe wengine waliokuwepo kwenye kikao hicho walichangia juu ya uimarishaji na uboreshaji wa elimu ikiwa ni pamoja na wazo la kuwa na mfuko wa Elimu wa Wilaya.
NZEGA TOWN COUNCIL (HALMASHAURI YA MJI NZEGA)
Sanduku la Barua: S.L.P 256 NZEGA-TABORA
Simu ya Mezani: +255677003373
Simu ya Mkononi: +255677003373
Barua Pepe: td@nzegatc.go.tz
Haki miliki zote zimehifadhiwa na nzegatc 2017