Wakazi wa Halmashauri ya Mji Nzega, wilaya ya Nzega Mkoa wa Tabora waendelea kunufaika na mahindi ya bei nafuu yanayotolewa na wakala wa Taifa wa hifadhi ya chakula ( NFRA). Ambapo kwa bei ya sokoni kilo moja ya mahindi huuzwa Tsh. 1000/= hadi 1150/= tofauti na bei kutoka hifadhi ya Wakala wa Chakula (NFRA) ambapo kilo moja ya mahindi huuzwa Tsh. 756/=
Afisa wa Udhibiti Ubora wa Mazao kanda Bw. Seth Gabriel amesema kuwa “Mahindi haya yameletwa kuwasaidia wananchi kukabiliana na Mfumuko wa bei za chakula nchini hivyo ni haki ya kila mwananchi kunufaika nayo kwani yame dhibitishwa na yana Ubora kwa matumizi ya binadamu”.
Akizungumza Bw. Nicodemus Hhando Afisa kilimo wa Halmashauri ya Mji wa Nzega amewataka wananchi kuwa wazi kusema pale ambapo kuna changamoto ili waweze kutatuliwa kwa haraka ili zoezi hilo liweze kufanyika bila kuwepo kwa kero kwa wanufaika hasa wanapohisi kilo ni Pungufu
Aidha wananchi wa Halmashauri ya Mji Nzega wameishukuru serikali kuwaletea mahindi haya ya bei nafuu kwani ya yameweza kuwapunguzia gharama za maisha kwa kuyanunua kwa bei ya tofauti na masoko ya kawaida.
NZEGA TOWN COUNCIL (HALMASHAURI YA MJI NZEGA)
Sanduku la Barua: S.L.P 256 NZEGA-TABORA
Simu ya Mezani: +255677003373
Simu ya Mkononi: +255677003373
Barua Pepe: td@nzegatc.go.tz
Haki miliki zote zimehifadhiwa na nzegatc 2017