Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Ndg. Philemon Magesa afungua kikao kazi cha siku moja kwa Walimu Wakuu wa Shule za Msingi na Sekondari,wakuu wa vituo vya Afya,wahasibu wa shule za msing,sekondari na vituo vya Afya kilichofanyika katika ukumbi wa Kanisa la KKKT-NZEGA tarehe 25/07/2018
Akifungua kikao hicho Mkurugenzi aliwashukuru na kuwapongeza wataalam hao kwa kuitikia wito kwa asilimia mia moja.”Nimefarijika kuona kuwa mmeitikia wito na mmefika kwa wakati,hili ni jambo jema sana mmeonyesha okamavu wa hali ya juu katika kazi.Nimefurahishwa sana kwa namna mlivyoitikia wito”Alisema Mkurugenzi
Mkurugenzi alieleza kuwa lengo kubwa la kikiao hicho cha kikazi ni kwaajili ya kupatia uelewa juu ya mambo mbalimbali hasa usimamizi wa fedha za miradi inayopelekwa katika maeneo yao.”Tumewaita hapa kwa sababu kubwa moja,kwanza kwa kutambua kuwa hamjapata mafunzo juu ya usimamzi wa fedha za miradi na hivyo kuwepo na changamoto mbalimbali, hivyo ili tuende sawa ni vizuri tukapa uelewa wa pamoja kwa maeneo kadhaa hasa katika usimamizi fedha za miradi ambayo imekuwa ikiletwa katika maeneo yenu” alisema Mkurugenzi
Mkurugenzi alitaja maeneo ambayo wanatakiwa kupata uelewa kuwa ni pamoja na;
Udhibiti na usimamizi wa fedha zinazopelekwa katika maeno yao.Mada hiyo iliwasilishwa na Kaimu Mweka hazina Bwa Emmanuel Mzile,ambapo alisema kwa fedha zote zinazopelekwa katika ngazi za vijiji lazima zisimamiwe na kutumika kulingana na miongozo pamoja na maelekezo yanayotolewa.
Usimamizi wa mikataba .Akifafanua alieleza kuwa lazima wajue mikataba hiyo ni ya namna gani wanayoingia anandaa nani,wajue vile vitu vya msingi vya mkataba alitolea mifano ya mikataba wanayoingia kama vile ya mafundi na vibarua hivyo ni vyema kujua anayeandaa huo mkataba ni mtaalam au mteja.Mada hiyo iliwasilishwa na Mwanasheria wa Mji Bi Ester Mlayda.
Usimamzi wa miradi.Alieleza kuwa mada hiyo itawasilishwa na Benard Bedda kwa niaba ya Mhandisi wa Ujenzi .Akitolea ufafanuzi alisema kuwa lengo kubwa la mafunzo hayo ni juu ya usimamizi wa miradi ikiwa na pamoja na ubora wa miradi.aliwataka washiriki kuhakikisha kuwa wanapata uelewa mpana juu ya eneo hilo na waulize maswali ili kuondokana na dukuduku walizonazo miyoni mwao.
Mada nyingine ilihusu nyaraka za malipo mbalimbali za malipo ambayo iliwasilishwa na Mkaguzi wa Ndani Bwana Omary Samizi.Akifafanua alisema kuwa nyaraka mbalimbali ambazo zipo kwenye malipo,maunuzi au mikataba.Alisistiza kuwa fedha za Serikali lazima zikaguliwe kuona value for money, lakini pia nyaraka za matumizi ya fedha hizo lazima ziwepo.
Swala la rushwa nalo ni swala la kuzingatia katika katika usimamizi wa miradi “unaingia mkataba lakini unajitengezea mazingira ya kula rushwa,unakuwa na intrest na ule mkataba”.Alisema Mkurugenzi.Mada hiyo iliwasilishwa na Kamanda wa TAKUKURU Wilaya ya Nzega.
Mada nyingine iliyowasilishwa ni pamoja na Sheria za Manunuzi ya Umma ambayo iliwasilishwa na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi Bwana Patrick Mgimwa ikifuatiwa na mada ya Uundaji wa Mabaraza ya Watoto iliyowasilishwa na Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Bwana Godson Harry.
Awali akimkaribisha Mkurugenzi Kaimu Elimu Msingi Bwana Ruben Nestory,aliwataka washiriki kuwa watulivu na kuhakikiksha wanaelewa juu ya mafunzo yanayotolewa .
NZEGA TOWN COUNCIL (HALMASHAURI YA MJI NZEGA)
Sanduku la Barua: S.L.P 256 NZEGA-TABORA
Simu ya Mezani: +255677003373
Simu ya Mkononi: +255677003373
Barua Pepe: td@nzegatc.go.tz
Haki miliki zote zimehifadhiwa na nzegatc 2017