Jumla ya Wanafuzi wa kike 190 wa kike wanaoishi katika mazingira magumu katika shule ya Sekondari Chief Ntinginya wamefadhaliwa na shirika lisililo la Kiserikali la CAMFED.
Akifafanua kuhusu ufadhili huo Mwakilishi wa shirika hilo ndugu Ezekiel Joseph alieleza kuwa Shirika linafadhili kiasi cha shilingi 250,000 kwa kila Mwanafunzi kwa mwaka,hivyo kila Mwanafunzi anaainisha mahitaji yake kulingana na kiasi cha fedha.Bwana Ezikiel aliyasema haya alipokuwa akigwa vifaa hivyo katika shule Chief Ntinginya hivi karibuni.
Kwa mwezi wa pili 2018 shirika limegawa vifaa vya kujifunzia,vyandarua ,sare za shule na baiskeli 26 kwa Wanafunzi 38.
Awamu nyingine ya ugawaji wa vifaa kwa Wanafunzi haoutafanyika baada ya taratibu kukamilika
Lengo kubwa ni kumlinda mtoto wa kike na kuhakikisha anakuwa salama na hatimaye kumaliza shule
NZEGA TOWN COUNCIL (HALMASHAURI YA MJI NZEGA)
Sanduku la Barua: S.L.P 256 NZEGA-TABORA
Simu ya Mezani: +255677003373
Simu ya Mkononi: +255677003373
Barua Pepe: td@nzegatc.go.tz
Haki miliki zote zimehifadhiwa na nzegatc 2017