WATOTO WAKIKE WENYE MAHITAJI MAALUMU KUANZA KUKAA BWENI
Watoto wakike wenye mahitaji maalumu Halmashauri ya Mji wa Nzega kuanza kukaa Bweni ,hili nikutokana na Ujenzi wa Bweni la Watoto hao linalo jengwa kwenye shule ya Msingi Nyasa 2 kufikia asilimia 98 ya ujenzi .hivyo kuleta matumaini kwa wazazi wa Watoto wenye mahitaji maalumu .
Juma Maganga (45) mkazi wa Mtaa wa Uswilu ana mtoto mwenye mahitaji maalumu anasema anaona tumaini jipya kwa mtoto wake kupata elimu bora ,mimi sina cha kusema na muombea kwa mwenyezi Mungu Maisha marefu Rais wetu kwani ametutendea jambo ambalo tusilo litarajia kabisa , mtoto wangu huwa kila siku namsukuma na baiskeli yake mpaka shule Kwenda na kurudi hivyo kupelekea kuchelewa kazini ,kukaa kwake Bwenini kutaniondoshea kuchelewa kazini na kugombana na bosi wangu kwa kuchelewa hivyo namshukuru sanaa Rais wangu namuombea kwa mwenyezi Mungu amlinde alisema
Bweni hili la Watoto wenye mahitaji maalumu lina uwezo wa kuhifadhi Watoto 80 kwa wakati mmoja ,na limegharimu kiasi cha Tsh. Milioni 128 ambazo ni fedha kutoka serikali kuu
NZEGA TOWN COUNCIL (HALMASHAURI YA MJI NZEGA)
Sanduku la Barua: S.L.P 256 NZEGA-TABORA
Simu ya Mezani: +255677003373
Simu ya Mkononi: +255677003373
Barua Pepe: td@nzegatc.go.tz
Haki miliki zote zimehifadhiwa na nzegatc 2017