Halmashauri ya Mji Nzega imetoa siku tatu kwa wazazi wenye watoto watoro kuhakikisha watoto hao wanarudi shuleni ili kuepuka hatua Kali za kisheria zitakazo chukuliwa dhidi yao.
Wito huo umetolewa leo na Onesmo Kisoka Katibu Tawala wa Wilaya ya Nzega kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya wakati akipokea maandamano ya kupinga utoro na kuhamasisha mahudhurio shuleni kwa kuzindua kauli mbiu ya "opareshen ya kamata weka ndani kwa kutotii amri halali" ambapo amesema kuwa kufuatia opareshen hiyo wanatoa msamaha kwa muda wa siku tatu kwa wazazi watakao chukua hatua ya kuwarudisha watoto wao shule na baada ya siku hizo kuisha watafanya msako nyumba kwa Nyumba na kuhakikisha wote wenye watoto watoro wanakamtwa na kufikishwa mahakamani.
Bwana Kisoka amefafanua kuwa wana orodha ya watoto wote watoro na wanachotakiwa kufanya ni kuwafuatilia na kuwafikisha wazazi wao kwenye vyombo vya sheria Ili watoto hao waweze kurudi shuleni na kupata haki ya kupata elimu ili waweze kuondokana na umasikini, ujinga na maradhi kwani elimu ni ufunguo wa maisha.
Alieleza kuwa katika halmashauri zote Mbili Halmashauri ya wilaya na ya Mji jumla ya wanafunzi mia 432 wa sekondari na wanafunzi elfu 1078 wa shule za msingi ni watoro ambapo amezitaka halmashauri kwa kushirikiana na serikali za vijiji kuhakikisha watoto wanapata chakula shuleni kwani kutokuwa na utaratibu huo kunadumaza maendeleo ya elimu na kuchochea utoro kwa wanafunzi.
Aidha akisoma taarifa, Mratibu wa maandamano hayo katika Halmashauri ya Mji, Bwana Hamdan Shemzigwa amesema kuwa halmashauri ya Mji ambayo ni mojawapi kati ya Halmashauri 8 za Mkoa wa Tabora na una jumla ya kata 10 ambapo una shule za msingi 34 zenye jumla ya wanafunzi elfu 21,813 wavulana wakiwa ni elfu 10,710 na wasichana elfu 11,103 na walimu 456 huku sekondari zikiwa 11 zenye wanafunzi elfu 4,557 wasichana 2,031 pamoja na wavulana 2,536 na jumla ya walimu mia 123.
Shemzigwa akisoma taarifa, aliema kuwa maandamano hayo yana lengo la kupinga utoro na kuhamasisha mahudhurio shuleni kwani utoro unaadhiri maendeleo ya Mtoto kitaaluma na kushindwa kufikia malendo ya watoto kupata elimu bora .
Ameeleza utoro kwa mji wa Nzega kwa shule za msingi ni jumla ya wanafunzi 91, wavulana wakiwa 44 na wasichana 47 na shule za sekondari jumla ni 112, wavulana 76 na wasichana 36 ambapo Mikakati iliyofanyika ni kuwabaini watoto kimadarasa na kwa majina ili kuweza kuwafuatilia wazazi na kuwachukulia hatua za kisheria na katika suala la mimba katika mji wetu kuna mimba 9, nne (4) zikiwa za shule za msingi na tano(5) zikiwa shule za sekondari ambapo zote zimeripotiwa katika vyombo vya sheria na kesi zinaendea kusikilizwa" Alisema
Alifafanua kuwa katika kuhakikisha Mtoto anafikia malengo yake kwa kumuepusha na vitendo kandamizi kila mwananchi anapaswa kutambua wajibu wake katika Jamii ambapo amewataka wazazi na walezi kufuatili mahudhurio ya watoto na kuhakikisha wanakagua maendeleo yao kitaaluma, kuwalea watoto wao katika maadili mema yanayokubalika na jamii, kuzungumza na watoto wao katika hatua mbalimbali za makuzi kupunguza na kudhibiti mihemko, kuwapatia watoto wao mahitaji muhimu kama vile chakula na mavazi ili kuwaepusha na vishawishi na hatimaye mimba za utotoni.
Bwana Shemzigwa akisoma taarifa hiyo kwa niaba ya Mkuu wa Idara ya Elimu Msing ametoa wito kwa Jamii kuzingatia sheria ya elimu namba 25 ya mwaka 1978 inayomtaka kila mwanafunzi aliyeandikishwa shule kuhudhuria masomo hadi atakapomaliza hivyo ni jukumu la kila mwananchi kusimamia hilo pamoja na kujiepusha na vitendo vya kumkandamiza Mtoto ili watoto waweze kufikia ndoto zao .
Pia ameiomba serikali kutimiza wajibu wake kwa kusimamia vizuri kanuni, Sera na miongozo dhidi ya vitendo hivyo kwa kuhakikisha wahusika wanawajibishwa ikiwa ni pamoja na kuendelea kuboresha miundo mbinu ya shule na kutatua changamoto ya upungufu wa walimu .
Sambamba na hayo pia ameishukuru serikali ya awamu ya tana kwa kuleta elimu bure, kuboresha miundo mbinu, kugawa vifaa vya kujifunzia na kufundishia pamoja na vifaa vya maabara kwa kupitia Sera ya elimu bila malipo..
Awali akimkaribisha Katibu Tawala wa Wilaya, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji alisema, maandamano hayo yamelenga kupinga ajira na utumikishwaji wa watoto katika kazi za majumbani, migodini, mashambani, kumbi za starehe, vilabu vya pombe, kuchungishwa ng'ombe pamoja na kupinga ukatili wa kijinsia na mimba za utotoni.
NZEGA TOWN COUNCIL (HALMASHAURI YA MJI NZEGA)
Sanduku la Barua: S.L.P 256 NZEGA-TABORA
Simu ya Mezani: +255677003373
Simu ya Mkononi: +255677003373
Barua Pepe: td@nzegatc.go.tz
Haki miliki zote zimehifadhiwa na nzegatc 2017