Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu tarehe 14.04.2018 alitembelea Halmshauri ya Mji Nzega kukagua utoaji wa huduma za Afya.
Akiwa ameambatana na Mkuu wa Mkao wa Tabora Ndg.Aggrey Mwanri,Mkuu wa Wilaya Ndg.Godfrey Ngupula,Mbunge wa Jimbo la Nzega Mjini Mhe. Mohamed Bashe,Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Nzega Ndg.Philemon Magesa pamoja na wataalam na wageni wengine mbalimbali,Mhe. Ummy Mwalimu alitembelea Kituo cha Afya Zogolo,Hospitali ya Wilaya ya Nzega ambayo iko katika eneo la Halmashauri ya Mji pamoja na Zahanati ya Mbogwe.
Akiwa katika kituo cha Afya Zogolo, Ummy Mwalimu aliweka jiwe la Msingi wa upanuzi wa ujenzi wa Kituo hicho.Kabla ya kuweka jiwe la Msingi alifanya ukaguzi wa ujenzi wa kituo hicho ambapo ailiridhika kwa kiasi kikubwa kwa kazi iliyofanyika.
Wakati akizungumza na Wananchi wa kata ya Nzega Ndogo aliwashukuru wananchi wa Nzega ndogo kwa mapokezi mazuri pamoja na ushiriki wao katika kuleta maendeleo.
Alisisitiza juu ya utoaji wa huduma bora za Afya na kwamba wakati Rais anaingia madarakani kituo cha Afya Zogolo ilikuwa na bajeti ya tshs 1.6 milioni lakini mpaka sahivi bajeti imepanda hadi kufikia tshs 15 millioni ni hizi ni fedha zinazotoka Wizara ya fedha.
Alisisitiza pia juu ya kujiunga na mfuko wa Bima ya Afya.
Alimshukuru Mkurugenzi kwa usimamizi mzuri wa tsh milioni 500 iliyotolewa kwaajili ya uboreshaji wa kituo cha Afya Zogolo na kuridhishwa na ujenzi uliofanyika.
Aliahadi kutafuta fedha kwaajili ya kujenga kliniki ya mama na mtoto katika kituo hicho.
Baadae alitembelea katika Hospitali ya Wilaya ya Nzega ambayo iko katika Halmashauri ya Mji wa Nzega aliweza kukagua utoaji wa huduma za Afya ambapo aliridhika na huduma zinazotolewa.
Pia alitembelea katika zahanati ya mbogwe ambapo alijionea huduma za Afya zinazotolewa .Akiwa katika kata ya Mbogwe alipokea taarifa ya Zahanati ya Mbogwe .Zahanati hiyo ni moja zahanati yenye nyota tatu katika Halmaashauri ya Mji Nzega.
Waziri Ummy Mwalimu alipokea kilio cha Wanambogwe ambapo waliomba zahanati hiyo ijengwe kuwa kituo cha Afya kwani wamekuwa wanasumbuka kufuata huduma mbali kutokana na jiografia ya Kata yao.
Waziri aliahidi kutafuta fedha kwaajili ya Ujenzi wa zahanati hiyo na kuwa kituo cha Afya.
NZEGA TOWN COUNCIL (HALMASHAURI YA MJI NZEGA)
Sanduku la Barua: S.L.P 256 NZEGA-TABORA
Simu ya Mezani: +255677003373
Simu ya Mkononi: +255677003373
Barua Pepe: td@nzegatc.go.tz
Haki miliki zote zimehifadhiwa na nzegatc 2017