Waziri wa kilimo na mbunge wa jimbo la nzega mjini amefanya ziara ya kukagua miradi katika jimbo lake la nzega Mjini.
Katika ziara yake aliyoifanya tarehe 18/10/2022 ametembelea jumla ya miradi mitatu 3 ambayo ni
Akiwa katika mtaa wa Utemeni kutembelea ujenzi wa shule ya msingi alimshukuru Mh. Rais Samia Hassan Suluhu kwa kutoa tshs milioni 200 (200,000,000) kwaajili ya ujenzi wa shule hiyo.Amesema shule hiyo ni muhimu kwani itawasaidia watoto waliokuwa wanaenda/kutembea umbali mrefu kupata elimu.Shule itakuwa na madarasa 9 pamoja na matundu ya vyoo
Amewashukuru wananchi wa mtaa huo kwa kukubali kutoa eneo la ujenzi wa shule na kulipwa fidia yenye jumla ya tshs 9,000,000 (milioni tisa).Amewashukuru pia kwa kujitolea kuchimba msingi kama nguvu kazi kutoka kwa jamii.Amewataka kuendelea na moyo huo wa kupenda elimu na kuwataka jamii nyingine Nzega kuigs mfano huo.
Akiongea na wananchi wa mtaa huo Mh.Bashe aliongeza kuwa kuna mkakati wa kuwawezeshs wanafunzi wanaomaliza kidato cha nne kufanya vizuri katika mitihani yao.Mkakati huo ni wa kuanzisha kempu (camp) katika shule ya Sekondari Bulunde ambapo kuna jumla ya walimu 20.Amewataka wazazi kutokuwa kikwazo cha cha kutowaruhusu wanafunzi kwenda camp.
Mh.Bashe amesema kuwa ili kukabiliana na upungufu wa chakula Serikali imetoa mahindi ambayo yatauzwa kwa tshs 750/= kwa kilo.
Amewataka wananchi wa Nzega kujiandiksha katika mfumo wa kielektronic kwaajili ya kupata mbolea ya ruzuku.amesisistiza kuwa yeye kama Mbunge atanunua mbegu ambayo itagawiwa kwa wananchi bure.mbegu hizo ni:
Amewataka Wananchi kuhakikisha wanatumia mvua za kwanza kwaajili ya kilimo.
Mh.Bashe ametaja aina nyingine za miradi ambayo inatekelezwa katika jimbo lake na hatua mbalimbali zilizofikiwa kama ifuatavyo:
Akiwa katika Kata ya Uchama katika kijiji cha Uchama Mh.Bashe ametembelea mradi wa ujenzi wa shimo la maji taka ambapo Meneja wa Mamlaka ya Maji Mjini(NZUWASA) Eng.Kilundumya amemweleza mbuge kuwa mradi huo umefikia 90% ya utekelezaji.Amesema kuwa Halmashauri ya Mji Nzega itakuwa ni Halmashauri ya pili kuwa na mradi huo baada ya Kahama.
Akizungumza na wananchi wa Uchama Mh.Bashe amemshukuru Mh.Rais kwa kutoa fedha kwaajili ya ujenzi wa mradi huo.Amewataka wananchi hao kutosikiliza longolongo badala yake waulinde mradi huo kwani una faida mbalimbali ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa mbolea.
Akiwa katika kata ya Mwanzoli, kijiji cha idudumo Mh.Bashe ametembelea mradi wa ukarabati wa ujenzi wa bwawa la IDUDUMO na kujionea shughuli zinazofanyika ikiwa ni pamoja na
Alimtaka mkandarasi kufanya yafuatayo;
Akiongea na wananchi wa Kijiji cha Idudumo amewahakikishia kuwa ahadi zote alizowaahidi kipindi cha kampeni atazitekeleza zote ikiwepo ahadi ya maji ambapo alimtaka Meneja wa Maji NZUWASA kuhakikisha kabla ya mwezi 12 mwaka 2022 maji yawe yameshafika katika kijiji hicho.
NZEGA TOWN COUNCIL (HALMASHAURI YA MJI NZEGA)
Sanduku la Barua: S.L.P 256 NZEGA-TABORA
Simu ya Mezani: +255677003373
Simu ya Mkononi: +255677003373
Barua Pepe: td@nzegatc.go.tz
Haki miliki zote zimehifadhiwa na nzegatc 2017